Mwanamke mmoja Michelle katika jimbo la Corolado
Marekani amepoteza kichanga chake baada ya mwanamke mmoja kumchoma kisu
tumboni na kuchukua kichanga chake kilichokuwa na miezi saba.
Dynel Catrece Lane ndiye
mwanamke ambaye ametajwa kuhusika na kosa hilo, alimchoma mwanamke huyo
kisu tumboni na kumtoa kichanga hicho halafu akakimbia kwenda Hospitali
akidai kwamba ametokwa ujauzito, wakati huo alikuwa amekishika kichanga
hicho mkononi kikiwa kimefariki.
Dynel Catrece Lane |
Baada ya Lane kufanya tukio hilo na kukimbia, Michelle alipiga simu ya dharura 911 kuomba msaada; “amenichoma tumboni.. nina ujauzito..“
Polisi wakiwa eneo la tukio |
Michelle alifikishwa Hospitali na kuendelea kupatiwa matibabu ya majeraha aliyochomwa kisu na mwanamke huyo.
Lane amefunguliwa mashtaka matatu, kosa la kuua, kutesa na kosa la kukiuka haki za watoto.
Social Plugin