Tuliwahi
kuandika stori ya mwanamke kujifungua watoto mapacha ambao walipishana
miezi miwili waliozaliwa katika moja ya hospitali huko Romania na
kuonekana kugusa hisia za watu wengi.
Hii
tena imetokea huko Uingereza baada ya mama mmoja kupata watoto wanne
ikiwa ni matokeo ya kushika ujauzito mara mbili ndani ya mwaka mmoja.
Sarah Ward mwenye umri wa miaka 29 alipata mapacha watatu ikiwa ni mwezi mmoja tangu ajifungue mtoto wake wa kwanza wa kiume,
Mwanamke huyo alijifungua mapacha hao
watatu ambao walizaliwa kabla ya muda huku mtoto wake wa kwanza akiwa
tayari na miezi nane.
Sarah amesema anashukuru kupata watoto
hao na amekua akitumia nepi zaidi ya 30 kwa siku kwa ajili ya
kuwabadilisha watoto wake lakini haoni kama ni gharama kutokana na
furaha aliyonayo.
Alisema
alipata wakati mgumu wakati akijaribu kushika mimba ya mtoto wake wa
kwanza na madaktari walipogundua ana mimba ya watoto mapacha watatu
walimshauri kumtoa mmoja ili watakaosalia waweze kukua vizuri lakini
alikataa na kutaka waache wote.
Social Plugin