Mwalimu wa shule ya Sekondari Kibasila, Gaudensia Albert aliyekuwa
akihifadhi kinyesi ndani kwake kwa miaka miwili amepelekwa Hospitali ya
Muhimbili baada ya daktari wa Hospitali ya Temeke kubaini ana matatizo
ya akili.
Mwalimu Mkuu Msaidizi wa Shule hiyo, Kyando amesema baada ya kugundulika kwa tukio hilo walimpeleka Hospitali ya Temeke kwa kuangalia afya yake ambapo daktari akasema ana tatizo la akili, wakamuhamishia Muhimbili.
Baada ya kufikishwa Muhimbili madaktari walimpatia dawa ambazo anatumia mpaka sasa pamoja na ushauri.
“Sisi bado tunamhitaji kutokana na tatizo la uhaba wa walimu wa sayansi ulioko nchini”—alisema Mwalimu Kyando na kuongeza kuwa mbali na tatizo la kukutwa na kinyesi bado mwalimu huyo alikuwa anafundisha vizuri.