Mabingwa watetezi wa klabu Bingwa barani Ulaya, Klabu ya Bayern Munich jana usiku wamefanikiwa kusonga mbele katika michuano hiyo baada ya kuifunga Shakhtar Donetsk jumla ya mabao 7-0.
Mabao ya Bayern Munich yamefungwa na Müller katika Dakika ya 4 kwa mkwaju wa penati ikiwa ni bao la kwanza kabla ya Boeteng kuandika goli la pili dakika ya 34.
Ribéry alifunga goli la tatu katika dakika ya 49, huku Muller akifunga kwa mara nyingine bao la nne dk51 na Badstuber alifunga bao la tano katika Dakika ya 63, Lewandowski akitupia la sita dakika ya 75 kabla ya Götze kumaliza kazi kwa kufunga bao la saba katika dakika ya 87.
Hadi mwamuzi anapuliza kipenga cha mwisho Bayern Munich wamefanikiwa kuondoka kifua mbele kwa jumla ya mabao 7-0.
Kwa matokeo hayo sasa Wajermani hao wanakuwa wametinga katika hatua ya Robo fainali ya Klabu bingwa Ulaya kwa ushindi huo.
Social Plugin