Matumizi ya kila siku ya dawa za
kupunguza maumivu kwa jina Paracetamol huongeza hatari ya ugonjwa wa
moyo ,kiharusi na kusababisha mtu kuaga dunia mapema ,utafiti umeonya.
Utafiti
huo umebaini kwamba wagonjwa wanaopewa dawa hizo za kupunguza maumivu
mwilini kwa mda mrefu wana hatari kubwa ya asilimia 63 kuaga dunia
haraka.
Hatari ya kupatikana na ugonjwa wa moyo iko juu kwa
asilimia 68 huku pia kukiwa na hatari kubwa ya asilimia 50 ya kupatikana
na vidonda vya tumbo ama hata kuvuja damu.
Paracetamol kama
zinavyojulikana hupendelewa sana na madaktari wengi wakidai ni salama
kushinda Aspirin, ambayo imehusishwa na kuvuja damu tumboni na Ibuprofen
ambayo imehusishwa na magonjwa ya moyo na kiharusi.
Lakini
watafiti wa Uingereza waliofanya uchunguzi huo uliowahusisha wagonjwa
666,000 wanasema kuwa hatari hiyo huenda ilipuuzwa na sasa wameagiza
uchunguzi ufanywe kuhusu usalama wa dawa hiyo.
Wanasayansi hao wanatoka katika taasisi ya matibabu ya Rheumatic and Musculoskeletal iliopo mjini Leeds.
Via>>BBC
Social Plugin