TAASISI ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu(NIMR),imesema vijana wenye umri wa kuanzia miaka 30 na kuendelea, wanaongoza kwa kutumia dawa za kuongeza nguvu za kiume.
Akizungumza
na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana,Mkurugenzi wa
NIMR,Dk.Mwele Malecela alisema kwa sasa tatizo hilo ni kubwa ambalo
linawakumba vijana wengi hususan barani Afrika.
Alisema
hali hiyo,imesababisha vijana hao kutafuta dawa za kuongeza nguvu za
kiume aina ya Mundex,ili waweze kupunguza ukubwa wa tatizo hilo.
“Vijana
wengi wenye umri wa kuanzia miaka 30 na kuendelea wana matatizo ya
upungufu wa nguvu za kiume, jambo ambalo limewafanya kutafuta dawa za
kuongeza nguvu ili waweze kuzitumia na kupunguza ukubwa wa tatizo.
“Tangu
tugundue dawa hii, idadi kubwa ya wanaokuja kununua ni vijana hasa
wenye umri wa miaka 30,hali ambayo inaonesha wazi kuwa tatizo hili
linakua kwa kasi,”alisema Dk Mwele.