Katika hali isiyokuwa ya kawaida na iliyowaacha midomo wazi watu wengi ni kwamba huduma katika kituo cha afya Nyankumbu Halmshauri ya mji wa Geita mkoani Geita zimesimama kwa muda wa masaa matatu na kusababisha wagonjwa waliokuwa hapo kuzidiwa na wengine kuzimia baada ya Matron wa kituo hicho na Nesi wake kuanza kutwangana makonde kwa kile kinachodaiwa kuwa ni wivu wa mapenzi.
Tukio hilo limetokea mwishoni mwa wiki iliyopita majira ya asubuhi ambapo Matroni na Nesi huyo ambao ni Wankyo Lyimo na Ritha Hanga waliotwangana
makonde muda mfupi baada ya kufika kazini hapo.
Inaelezwa kuwa nesi na matroni huyo walikuwa wanatuhumiana kuchukuliana mabwana.
Shuhuda
mmoja ambaye hakutaka jina lake litajwe ameiambia Malunde1 blog kuwa ,wahudumu hao wa kituo cha Afya walifika kama kawaida kazini lakini kila mmoja alikuwa amefura hasira dhidi ya
nyoka mwenye sumu kali.
"Walifika
kama kawaida kazini, lakini kilichotushangaza ni kuona kila mmoja akiwa na hasira kali ,hali hiyo ilitufanya hata sisi kuwa na mashaka makubwa juu yao'
"Muda mfupi walianza kutupiana vijembe jambo ambalo lilisababisha wagonjwa
waliokuwepo kuanza kushangaa na wengine walikuwa na hali mbaya kuzimia kwa muda
mfupi",alieleza shuhuda huyo.
Baadhi ya wagonjwa walisema wameshangazwa na kitendo hicho cha Matroni na Nesi wake kutupiana
vijembe mpaka kutwangana makonde na kudai kuwa si jambo la busara hata kidogo kupigana ngumi hivyo wachukuliwe
hatua.
Alipotafutwa
Matroni na nesi wake ili kutaka kujua chanzo cha kutwangana makonde kazini walidai
wao siyo wasemaji bali msemaji ni mganga mkuu wa Hospitali.
Kaimu Mganga
mkuu aliyejulikana kwa jina moja la Mshandete
alikiri kuwepo kwa tukio hilo lakini akasema limekwisha kupelekwa kwa afisa
utumishi na hawezi kulizungumzia.
Naye Afisa
utumishi mmoja pamoja na kugoma kutaja jina lake aliyekutwa Ofisini na kuulizwa
juu ya suala hilo alikiri kuwepo kwa sakata hilo lakini akasema haoni haja ya
kulifuatilia kwani ni jambo dogo.
"Jambo hilo
lipo lakini sioni ukubwa wake kwa nini ufuatilie suala dogo kama hili? kuna mambo
mengi ya kufuatilia wewe nenda ufuatilie mengine ",alisema afisa huyo.
Habari za
kuaminika kutoka ndani ya kituo hicho zinasema pamoja na wauguzi hao kuanza
kutupiana vijembe muda mrefu lakina hakuna hata kiongozi wa juu aliyechukua
hatua dhidi yao.
Na Valence Robert- Malunde1 blog Geita
Social Plugin