Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

Hii Kali !! MBWA ATEMBEA MTAANI KWA MIGUU MIWILI KAMA BINADAMU AKIWA AMEVAA SKETI NA BEGI LA MADAFTARI KAMA MWANAFUNZI

 

Mbwa aliyekuwa amevaa kama binadamu huku akitembea kwa miguu yake miwili amezua mjadala katika mitandao na watu kumgeukia kila kona anayokatiza.

Tukio hili limetokea huko Kusini Magharibi mwa China hasa jimbo Sichuan.

Mbwa huyo mwenye umri wa mwaka mmoja ambaye ni dume mwenye manyoya ya kutosha, alionekana akiwa amevalia kofia,shati na sketi.

Mbwa huyo alikuwa akitembea huku mgongoni akiwa na begi la shule kwa hakika alikuwa na muonekano wa mwanafunzi mdogo wa jinsi ya kike.

Alikuwa na muonekano maridadi na mvuto hasa.

Na huwezi kuamini kuwa anaweza kutembea kwa miguu miwili ya nyuma anasema mpita njia Luo.

Mmiliki wa mbwa huyo Zhu anasema ametumia muda wa muda wa mwezi mmoja kumfundisha mbwa huyo kutembea wima.

Wakati akivalishwa nguo mbwa huyo alionekana kuwa mtulivu na kuruka ruka na ana uwezo wa kutembea kilomita mbili wima kama mwanadamu.

Zhu anasema alianza kumfundisha mbwa huyo kama kujifurahisha yapata miaka ishirini iliyopita na baada ya mafanikio hayo, anawafundisha mbwa wengine wengi na wa umri tofauti tofauti .
Via>>BBC

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com