Vurugu kubwa imetokea katika mji mdogo wa Mererani wilayani Simanjiro
baada ya waendesha bodaboda na wakazi wa mererani kufanya maandamano na
kufunga barabara ya kia Mererani kwa madai ya kupinga hatua ya Jeshi
la Polisi kuwanyanyasa waendesha boda boda hali iliyolilazimu Jeshi la
Polisi kurusha mabomu ya machozi na kujeruhi baadhi ya watu.
ITV ilifika katika mji mdogo wa Mererani na kushuhudia vurugu hizo
na baadhi ya watu waliyojeruhiwa huku wakazi wa Mererani wakililaumu
jeshi la polisi kwa kuwanyanyasa waendesha bodaboda ambao wanadaiwa
kutovaa kofia ngumu lakini wanakatwa hata waliyopo kanisani msikitini na
kwenya bar wakati pikipiki zimepaki na kukilipishwa faini kubwa na mtu
mmoja ukamatwa zaidi ya mara tatu kwa wiki.
Akizungumzia vurugu hizo mwenyekiti wa mamlaka ya mji mdogo wa
Mererani Albert Siloli amesema hakubalini na operesheni hiyo kwani jeshi
limetumia nguvu kubwa sana bila sababu huku diwani wa kata ya Intiamtu
Lucas Zacharia akidai kuwa hali hiyo imesababishwa na jeshi la polisi
kufanya kazi bila kushirisha viongozi wa maeneo husika na huo siyo
utawala pia haupaswi kufumbiwa macho.
Mbunge wa simanjiro Christopher Ole Sendeka amelitaka jeshi la
polisi makao makuu kufanya uchunguzi dhidi ya askari wake wanaotuhumiwa
kufanya matendo yasiyo na nidhamu kwa jeshi ilo yanayo ongezeka kila
kukicha bila huruma.
Akizungumza kwa njia ya simu kamanda wa polisi mkoa wa manyara
Christopher Fuime amesema Jeshi la polisi lilikuwa katika operesheni ya
kawaida lakini wananchi walifanya vurugu na kusababisha kutokea kwa hali
hiyo lakini hawakuwa na lengo la kumdhuru mtu yeyote.
Via>>ITV