Baadhi
ya waathirika wa mvua ya Mawe katika kijiji cha Mwakata wilaya ya Kahama
mkoani Shinyanga wamelazimika kuifunga barabara ya Isaka -Kahama na
kuathiri kwa muda mawasiliano katika nchi ya Rwanda,Burundi na Uganda
wakishinikiza serikali kuwagawia chakula,magodoro,branketi,mahema na
shuka baada ya kunyeshewa na mvua usiku wakati vifaa vya misaada vikiwa
vimefungiwa kwenye maghara hali iliyosababisha jeshi la polisi kuwatawanya wananchi kwa mabomu ya machozi na kufungua njia ili gari ziendelee na
safari.
Vurugu hizo zimedumu saa moja ambapo kundi la wananchi wenye
hasira wakiilalamika kamati ya maafa kwa kushindwa kuwahudumia waathirika
kwa wakati hali iliyosababisha waathirika wanaolala nje kunyeshewa mvua
huku wakinamama wakila ani nguvu kubwa iliyoumika kutuliza ghasia
zilizosababisha watoto kupotea kutokana na mabomu ya machozi
yaliyotumika kutawanya wananchi waliofunga barabara.
Kufuatia vurugu hizo mbunge wa jimbo la Msalala Mh.Ezekiel Maige
amelazimika kufika kwenye eneo la tukio na kujionea hali halisi ambapo
amewasihi wananchi kuwa watulivu wakati akifanya mipango ya kuzungumza
na kamati ya maafa ili iweze kutoa vifaa vinavyolalamikiwa na
vigawiwekwa walengwa.
Alipotakiwa kujibu malalamiko hayo katibu wa maafa wilaya ya Kahama
ambaye ni mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya ushetu kahama
Bi.Isabela Chilumba amesema vurugu hizo zinasababishwa na wanasiasa na
kwamba kamati ya maafa imeba ini kuna kundi la vijana kutoka vijiji
jirani wakivizia chakula na vifaa vya misaada.
Naye mkuu wa mkoa wa shinyanga Bw.Ally Nasoro Rufunga amekabidhi
misaada hiyo kwa wenyeviti wa serikali za vitongoji na vijiji pamoja na
kutoa fedha zaidi ya shilingi milioni nne kwa kaya 14 ambapo kila
familia iliyofiwa imepatiwa kiasi cha shilingi laki tatu kama pole ya
rambirambi ya serikali ya mkoa wa shinyanga na kuahidi kusaidia zaidi
kadri misaada inavyopatikana.
Via>>ITV
Social Plugin