VURUGU ZA WAATHIRIKA WA MAAFA YA MVUA KUFUNGA BARABARA ZATAJWA KUSABABISHWA NA WANASIASA


Baadhi ya waathirika wa mvua ya Mawe katika kijiji cha Mwakata wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga wamelazimika kuifunga barabara ya Isaka -Kahama na kuathiri kwa muda mawasiliano katika nchi ya Rwanda,Burundi na Uganda wakishinikiza serikali kuwagawia chakula,magodoro,branketi,mahema na shuka baada ya kunyeshewa na mvua usiku wakati vifaa vya misaada vikiwa vimefungiwa kwenye maghara hali iliyosababisha jeshi la polisi kuwatawanya wananchi kwa mabomu ya machozi na kufungua njia ili gari ziendelee na safari.

Vurugu hizo  zimedumu saa moja ambapo kundi la wananchi wenye hasira wakiilalamika kamati ya maafa kwa kushindwa kuwahudumia waathirika kwa wakati hali iliyosababisha waathirika wanaolala nje kunyeshewa mvua huku wakinamama wakila ani nguvu kubwa iliyoumika kutuliza ghasia zilizosababisha watoto kupotea kutokana na mabomu ya machozi yaliyotumika kutawanya wananchi waliofunga barabara.
Kufuatia vurugu hizo mbunge wa jimbo la Msalala Mh.Ezekiel Maige amelazimika kufika kwenye eneo la tukio na kujionea hali halisi ambapo amewasihi wananchi kuwa watulivu wakati akifanya mipango ya kuzungumza na kamati ya maafa ili iweze kutoa vifaa vinavyolalamikiwa na vigawiwekwa walengwa.
Alipotakiwa kujibu malalamiko hayo katibu wa maafa wilaya ya Kahama ambaye ni mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya ushetu kahama Bi.Isabela Chilumba amesema vurugu hizo zinasababishwa na wanasiasa na kwamba kamati ya maafa imeba ini kuna kundi la vijana kutoka  vijiji jirani wakivizia chakula na vifaa vya misaada.
Naye  mkuu wa mkoa wa shinyanga Bw.Ally Nasoro Rufunga amekabidhi misaada hiyo kwa wenyeviti wa serikali za vitongoji na vijiji pamoja na kutoa fedha zaidi ya shilingi milioni nne kwa kaya 14 ambapo kila familia iliyofiwa imepatiwa kiasi cha shilingi laki tatu kama pole ya rambirambi ya serikali ya mkoa wa shinyanga na kuahidi kusaidia zaidi kadri misaada inavyopatikana. 
Via>>ITV

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
أحدث أقدم