Pamoja na kukataa kwamba hakumtemea mate mshambuliaji wa New Castle Papis Cisse, beki wa Man United, Jonny Evans amefungiwa mechi sita na Shirikisho la soka England FA.
Naye Papis Cisse amefungiwa michezo saba na Shirikisho hilo.
FA imetoa adhabu hiyo baada uya
kuthibitisha kupitia mkanda wa video hiyo katika mchezo uliochezwa
jumatano iliyopita katika uwanja wa St. James Park ambapo Man U waliibuka na ushindi wa goli 1-0, goli lililofungwa na Ashley Young.
Adhabu hiyo itamfanya beki huyo kukosa
mchezo wa robo fainali dhidi ya Arsenal siku ya jumatatu kwmenye uwanja
wa Old Tranford na michezo mingine atakayoikosa ni ile dhidi ya Tottenham, Liverpool, Aston Villa, Manchester City, na Chelsea.
Kwa upande wa Cisse atakosa michezo dhidi ya Everton, Arsenal, Sunderland, Liverpool, Tottenham,Swansea na Leicester
Social Plugin