Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

WACHUNGAJI NAO WAMVAMIA LOWASSA, WAUNGWANA WAMEPONDA, WADAI NI "USANII MTUPU",JANUARI MAKAMBA ALIPUKA!!


Name:  ImageUploadedByJamiiForums1427101586.450986.jpg
Views: 0
Size:  83.8 KB


Name:  ImageUploadedByJamiiForums1427101603.403622.jpg
Views: 0
Size:  76.4 KB


Leo katika Hali isiyo ya kawaida wachungaji wavamia Eneo la Area D ambapo ni Makazi ya viongozi mbali mbali wakimsaka Edward Lowassa. viongozi hao wa dini walikuwa na shauku kubwa na nyuso za furaha wakiimba nyimbo za matumaini Mapya na Edward lowassa.
Aidha misururu hio imesababisha Ndugu Samwel Sita kusubiri kwa Muda kupisha viongozi hao kwenda kuiona nuru ya MATUMAINI. pia ilimuwia vigumu ndugu Fredric Sumaye kuwahi appointments yake na Spika wa Bunge kupisha msafara takatifu kwenda Jirani yake Edward Lowassa.
Mambo yanazidi kupamba moto kuelekea nuru ya matumaini kwa Watanzania ambao mara zote wamuonapo Edward Lowassa hupata faraja.
Wachungaji hao wametabiri na kuahidi kunena kwa vitendo, na mpaka sasa bado wanaendelea kujieleza ni nini wanacho muahidi bwana Edward Lowassa kama balozi wamuaminiye katika safari ya MATUMAINI.

Malunde1 blog imepitia baadhi ya Mitandao ya kijamii,Fuatilia hapa chini UONE TULIOCHOKUTANA NACHO

    filamu za Edward Lowasa lowasa zinaendelea
    baada ya masheikh feki kwenda nyumbani kwa lowasa,baadaye bodaboda sasa ni wale wachungaji aliokuwa anatembelea makanisa yao na kuwaachia maburungutu ya pesa leo wametinga nyumbani kwake kumuomba agombee urais.

    watu hao waliojiita wachungaji wamefika nyumbani kwa lowasa wakiwa na mabango ya kumuomba agombee urais na aliyekuwa akiratibu kuwakusanya wachungaji hawa feki kwenda kwa lowasa ni mwenyekiti wa ccm mkoa wa shinyanga akishilikiana na mwenyekiti vijana ccm mkoa wa arusha,mwenyekiti ccm wilaya ya monduli na wajinga wengine.

    Dini zimeingiliwa viongozi waliowengi wa dini wameendekeza njaa na ndio maana wengine wapo kwenye sakata la ESCROW maana wapo kwa ajili ya pesa nchi inaendelea kulaaniwa.


    wachungaji na maaskofu wa ukweli ni wale waliopitisha waraka kwenye makanisa yao yote nchi nzima ya kuwahamasisha waumini kujiandikisha na kuikataa katiba pendekezwa ya ccm lakini hawa wanaoenda kwa lowasa muwachunguze vizuri akili zao kama wana akili nzuri maana ata shetani ana wafuasi.pia muwaangalie vizuri kama kweli ni wachungaji maana juzi masheikh kumbe walikuwa feki waliwachukua wafuasi wa ccm na kuwavalisha makanzu waigize kama masheikh.


    "filamu za Edward Lowasa lowasa zinaendelea
baada ya masheikh feki kwenda nyumbani kwa lowasa,baadaye bodaboda sasa ni wale wachungaji aliokuwa anatembelea makanisa yao na kuwaachia maburungutu ya pesa leo wametinga nyumbani kwake kumuomba agombee urais.
watu hao waliojiita wachungaji wamefika nyumbani kwa lowasa wakiwa na mabango ya kumuomba agombee urais na aliyekuwa akiratibu kuwakusanya wachungaji hawa feki kwenda kwa lowasa ni mwenyekiti wa ccm mkoa wa shinyanga akishilikiana na mwenyekiti vijana ccm mkoa wa arusha,mwenyekiti ccm wilaya ya monduli na wajinga wengine.
Dini zimeingiliwa viongozi waliowengi wa dini wameendekeza njaa na ndio maana wengine wapo kwenye sakata la ESCROW maana wapo kwa ajili ya pesa nchi inaendelea kulaaniwa.
wachungaji na maaskofu wa ukweli ni wale waliopitisha waraka kwenye makanisa yao yote nchi nzima ya kuwahamasisha waumini kujiandikisha na kuikataa katiba pendekezwa ya ccm lakini hawa wanaoenda kwa lowasa muwachunguze vizuri akili zao kama wana akili nzuri maana ata shetani ana wafuasi.pia muwaangalie vizuri kama kweli ni wachungaji maana juzi masheikh kumbe walikuwa feki waliwachukua wafuasi wa ccm na kuwavalisha makanzu waigize kama masheikh."
    MWINGINE HUYU HAPA CHINI
 Kule JAMII FORUMS NAKO HAPATOSHI,NIMEKUTANA NA HII
Wakati huu tunapoelekea kwenye uchaguzi mkuu, ilikuwa ni kipindi muafaka cha kujiuliza tulikosea wapi, ili tujirekebisha na kujenga misingi imara ya Taifa letu! Misingi itakayoweka kikomo cha kujiuliza kwa nini nchi hii ina kila kitu lakini bado ni maskini?

Misingi ya kuwa na viongozi bora! Viongozi wazalendo! Wanaojua kuwa uongozi ni dhamana na sio sehemu ya kwenda kutajirika na kulipa fadhila! Viongozi ambao wameamua kuacha maisha rahisi ya kuttumikiwa, na kukubali kujitolea kuwa watumishi wa taifa zima! Walio tayari kubeba mzigo wa Umasikini wetu, elimu yetu duni, huduma mbaya za afya, na uduni kama taifa!


Cha kusikitisha, tunafanya usanii kweupeee! Anayefanya huo usanii anajua kuwa ni usanii. Na sisi wananchi ambao mwisho wa siku ndio tutakaoumia, tunajua kuwa ni usanii, halafu tunashangilia kwa pamoja! Tukitegemea kuwa mwisho wa usanii huu taifa letu litasonga mbele!


Huhitaji kuwa mtaalamu wa sayansi ya siasa kujua kuwa kuna baadhi yetu tumenunuliwa kwa vipande vichache vya fedha ili ku-support usanii huu. Baadhi ya Waandishi pamoja na chumba chote cha habari kimenunuliwa! Baadhi ya viongozi wa dini wamenunuliwa! Makundi ya watu wenye mahitaji maalumu wamenunuliwa! Makundi ya vijana, akina mama na sasa mpaka wanafunzi wamenunuliwa!


Aliyenunua anajua kuwa kanunua, aliyenunuliwa anajua kuwa kanunuliwa, na tusionunuliwa tunajua kuwa wenzetu wamenunuliwa na wote tuko kimyaaaa! Ndugu zangu tutalipa gharama kubwa sana kwa huu usanii tunaoufanya!


Tunatengeneza mazingira ya kuonekana kwamba tumeombwa kugombea Udiwani, Ubunge na sasa Uraisi kwa kutengeneza maigizo! Tunacheza na future yetu na ya watoto wetu!


Pesa zinatumika kukusanya watu, kuwasafirisha, kuwapa chakula na malazi, per diem, na hawa masikini ETI wamechanga pesa za kukupa ukagombee! Tuache hii jamaniii... Tuwe serious kwenye hili. Huko walikoendelea hawafanyi hivi! Tafadhali.


Hatutegemei ukagombee kutuongoza, kuwa mtumishi wetu kwa kuombwa. Tunategemea uko tayari kututumikia baada ya wewe mwenyewe kujipima, ukaona kuwa uko tayari na unaweza. Unajua matatizo yetu, na una dira ya mwelekeo wetu kama taifa!

TUACHE USANII.



====
KAULI YA Januari Makamba=====
Quote By January Makamba
Nafasi ya Urais ni nafasi ya hadhi na heshima kubwa. Unapoiomba hupaswi kufanya michezo ya kuigiza. Huu utaratibu wa kuratibu watu, kuwasafirisha, kuwapa posho na ubwabwa waje kukuomba kugombea ni michezo ya kuigiza ambayo ni aibu kubwa.

Kila mgombea ana uwezo wa kutengeneza WATU wa kumuomba kugombea lakini wengine hatufanyi hivi kwasababu tunaheshimu nafasi tunayoiomba na tunaamini kwamba haipaswi kutafutwa kwa ulaghai na maigizo.

Ni aibu sana kutumia shida na njaa za watu kisiasa. Ni aibu sana kukusanya vijana na wazee wa watu na kuwapangia viti na mahema na kuwapa pesa halafu pesa na kuwapiga picha. Ukiona mtu anatafuta nafasi ya uongozi kwa ujanja na ulaghai ujue atatawala kwa ujanja na ulaghai.

Viongozi wanaokubalika na watu hawangaiki kupanga Viti na mahema na kuwapiga picha watu wanaowakubali.

Mgombea anayehaha na kutumia pesa nyingi kuonyesha anakubalika ukweli ni kwamba hajiamini. Kama unakubalika huwezi kuratibu makundi na kuyalipa na kuwapiga picha na kuita waandishi wa habari waje kushuhudia. Hizo ni mbinu za mfa maji.

Naamini Chama changu hakitatishwa na nguvu za maigizo. Tunataka uongozi safi unaomuogopa mungu. Tunataka uongozi wenye uadilifu na fikra mpya za kuisogeza mbele Tanzania. Tunataka viongozi watakaomaliza shida za Watanzania sio wanaozitumia shida hizo kisiasa.

Hata Mzee Makamba, pamoja na umri wake wa miaka 75, leo akiwa na pesa za kumwaga anaweza kutengeneza makundi yakamuombe kugombea Urais.

Ifike mahali katika nchi yetu tuache hii michezo. Tukiendelea na mambo haya, tunatengeneza taifa linaloendeshwa kwa propaganda tu. Watu wanaotaka kuomba nafasi ya Urais wanapaswa kuwa na ujasiri na wanapaswa kujiamini na kusema wanataka nafasi hiyo na wana fikra gani mpya bila kutumia pesa kuonyesha kwamba wanagombea kwasababu wanahitajika na watu. Uongozi thabiti na shupavu hautokani na michezo ya kuigiza.

January Makamba

SOMA ZAIDI HAPA 

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com