Mahakama kuu ya Tanzania katika kikao chake kilichofanyika mkoani Geita imewatia hatiani na kuwahukumu kunyogwa mpaka kufa, watuhumiwa wa nne wa mauaji ya mtu mwenye ulemavu wa ngozi Zawadi Magindu aliyeuwawa mwaka 2008 katika kijiji cha Nyamalulu wilayani.
Awali akisoma shitaka hilo mbele ya jaji wa Joacqune Mello
mwanasheria wa Serikali Eziloni Mwasimba aliambia mahakama hiyo kuwa mnamo tarehe
11.03 .2008 majira ya saa moja jioni washitakiwa 4 ambao ni Masalu Kahindi, Ndalanya Rumora, Singu
Siantemi, na Nasoro Saidi, huko katika kijiji Nyamalulu Wilayani Geita walimuua kwa
kumkata mapanga na kusababishia kifo kilichotokana na kuvuja damu nyingi.
Eziloni aliongeza kuwa watuhumiwa hao baada ya kutenda unyama
huwa walikimbilia sehemu mbalimbali za vijiji vingine ili wasikamatwe na mkono wa sheria hivyo akiomba
Mahakama kutoa hukumu kali dhidi ya watuhumiwa ili liwe fundisho kwa watu wengine
wenye nia kama hiyo.
Mara baada ya kusikiliza ushahidi wa pande zote bila kuacha shaka
lolote ndipo mahakama hiyo kwa kutumia kifungu cha sheria 196 na 197 ya kanuni ya
adhabu sura ya 16 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2002.
Kwa mujibu wa mashahidi waliojitokeza inasemekana mtuhumiwa namba
mbili Ndahanya Lumola na mtuhiwa namba tatu Singu Siantemi ndio
waliohusika na upimaji wa mifupa ya marehemu Zawadi ambapo hutumia wembe
na shilingi moja kuweka karibu na mifupa ya Albino ili kujua kama
itavuta kama sumaku na kipimo kingine ni redio ambayo huiweka karibu na
mifupa na ikizimika ndio mifupa hiyo huonekana kuwa na ubora tofauti na
hapo mifupa hiyo huwa haifai na hutupwa.
Mashahidi hao wamesema vipimo hivyo havina uhalisia wa aina yoyote kwani hakuna binadamu mwenye mifupa inayokuwa na sumaku.
Kwa kuzingatia ushahidi na utetezi wa pande zote jaji Joaquine
De-mello amesema mahakama imejiridhisha pasipo kuacha shaka yoyote kuwa
watuhumiwa wote wanne walihusika na mauaji ya Bi Zawadi Magindu katika
kijiji cha Nyamalulu wilayani Geita mnamo tarehe 11 mwezi wa tatu mwaka
2008 usiku.
Aidha jaji De-mello amesema anashangazwa na kesi zote alizosimamia
zinazohusu mauaji ya Albino watuhumiwa wote wanaofikishwa mahakamani ni
wakataji wa mapanga na kuhoji wakataji hao wanapeleka wapi mifupa hiyo?
Na kuwataka wahusika kuhakikisha wanawapata wanunuzi na watumiaji wa
viongo hivyo vya watu wenye ulemavu wa ngozi.
Hata hivyo baada ya hukumu hiyo kutolewa baadhi ya wananchi waliokuwa mahakamani
akiwemo mwenyekiti wa walemavu wa ngozi mkoa wa Geita na wengine wenye ulemavu mbali na kuipongeza mahakama
kwa kutoa hukumu ya haki inayoashiria kuwapa ulinzi jamii hiyo ya
maalbino pia wamesema mahakama
haikutenda haki kwani kuna watuhumiwa wengi walitajwa kwenye kesi hiyo lakini hawakuonekana
mahakamani.
Na Valence Robert-Malunde1 blog Geita
Social Plugin