Wakuu wa jimbo la Bihar, India,
wamewakamata mamia ya watu na wamewafukuza wanafunzi zaidi ya 750 baada
ya video kutanda mtandaoni, zinazoonesha wanafunzi wakidanganya wazi
kwenye mtihani wa kumaliza shule.
Baadhi ya wazee na askari polisi wamekamatwa, na mitihani ijayo katika vituo vine imeahirishwa.
Picha
hizo zinaonesha wanaume wakiparamia kuta za vituo vya mitihani na
kuwakabidhi wanafunzi majibu, na wanafunzi wengine wakikopi kutoka
maelezo hayo.
Social Plugin