Amini usiamini wanasayansi nchini Marekani wameanza mikakati ya kusafisha dhahabu kutoka kwa kinyesi cha watu.
Kwa mujibu wa ripoti moja watafiti hao wanasema kiwango cha dhahabu na madini mengine nadra na yenye thamani ya juu kwenye vituo vya kusafishia kinyesi inazidi idadi ya utafiti unaofanywa katika katimbo nyingi za dhahabu.
''Kiwango
cha dhahabu hapa ni cha juu zaidi ya viwango vinavyotumiwa na watafiti
kubaini iwapo mgodi una madini hayo ya kutosha au la''
Ripoti hiyo
imechapishwa katika kongamano la 249 la wanakemia wa Marekani ''
American Chemical Society (ACS) iliyoandaliwa huko Denver Marekani .
Kulingana
nao iwapo kutatambuliwa mbinu ya kusafisha kinyesi na kuitenga dhahabu
atakayegundua mbinu hiyo ataisaidia sana mazingira.
Daktari
Kathleen Smith, aliyesaidia katika uandishi wa ripoti hiyo alisema kinyesi cha
watu kina kiwango cha juu mno cha dhahabu, fedha ,palladium na vanadium.
'' Madini hayo ya vanadium shaba yana manufaa makubwa sana katika
utengenezaji wa bidhaa zinazotumika katika simu za mkononi na kompyuta
mbali na bidhaa mbalimbali za kielektroniki.
Marekani huwa inasafisha zaidi ya tani milioni saba ya kinyesi kila mwaka kulingana na dakta Dr Smith.
Nusu
ya uchafu huwa hutumika tena kutengeneza mbolea katika misitu huku nusu
iliyosalia ikitumika kurejesha ubora wa ardhi baada ya kuchimbwa kwa
madini tofauti tofauti nchini humo.
Watafiti hao wanatumia mbinu maalumu inayotumia kemikali ifahamikayo kama '' leachates'' kufyonza madini kutoka kwenye mawe.
Utafiti
huu unatilia pondo utafiti wa awali uliodai kuwa kinyesi kutoka kwa
wamarekani milioni moja inazaidi ya dhahabu na madini yenye thamani ya
dola milioni 13.
via>>BBC
Social Plugin