Watu
watatu wamefikishwa mahakama ya wilaya ya Chato kusomewa shitaka la
mauaji ya mtoto Yohana Bahati aliyeibiwa hatimaye kuuwawa tarehe 15
Februali katika kitongoji cha mapinduzi wilayani Chato mkoani Geita.
Akizungumza na waandishi wa habari, kamanda wa polisi mkoa wa Geita
Sacp Joseph Konyo amesema watu wengine wawili bado wanahojiwa na jeshi
la polisi ili kupata ushahidi unaojitosheleza katika kesi hiyo,
amewataja watu waliofikishwa mahakamani ni Bahati Misalaba ambaye ni
baba wa Yohana, Juma Lupembe Kilebelo, Manyanda Mandege almaarufu
Makongoro mkazi wa wilaya ya Mbogwe na mchimbaji wa dhahabu.
Kamanda konyo amesema jeshi la polisi linaendelea na juhudi za
kuwakamata wauwaji wa kukodiwa wanaofanya mauaji hayo kwa ujira mdogo wa
laki moja ili kudhibiti vitendo vya mauaji katika maeneo ya kanda ya
ziwa.
Katika tukio jingine jeshi la polisi limefanikiwa kuwakamata na
kuwafikisha mahakamani watu watatu wanaosadikika kuwa ni majambazi
wazoefu wa kuteka magari barabarani na kuvamia maduka ya fedha mkoani
Geita, watu hao Niosca John Bosco, Kapuru Msigwa ustaadhi, na Elias
Shigilimelo Bambala.
via>>ITV
via>>ITV