WATU
watano wa familia moja katika Kitongoji cha Benaco, Kata ya Mtandi
Halmashauri ya mji wa Masasi mkoani Mtwara, wamelazwa katika Hospitali
ya Mkomaindo huku hali zao zikiwa mbaya baada ya kunywa dawa ya kienyeji
waliyopewa na mganga wa tiba za asili.
Dawa
hiyo ya kienyeji inaitwa nyungu, ambayo hutokana na mchanganyiko wa
majani tofauti ambayo hupondwa kwenye kinu na kuchanganywa na maji na
kuchemshwa.
Mgonjwa hufunikwa kwa nguo nyeupe na kufukizwa na mvuke wa maji hayo kisha huyanywa.
Mkuu
wa Polisi wa Wilaya ya Masasi, Azaria Makubi, alitaja wanafamilia
waliolazwa hospitalini ni baba wa familia hiyo Geofrey Evance (43), mke
wake, Hadija Salumu (30), dada yake Fidea Evance (40) pamoja na watoto
wake wawili, Husna Zuberi (8) na Godfrey Geofrey (10).
Imeelezwa
baada ya wanafamilia hao kunywa dawa hiyo, wote hali zao zilibadilika
ghafla huku baadhi wakitokwa mapovu vinywani na baadae walipoteza fahamu
na kukimbizwa katika hospitali ya Mkomaindo ambako wamelazwa hadi sasa.
Makubi
alithibitisha tukio hilo na kusema ni la juzi saa 12:30 jioni katika
eneo la Makondeko, Halmashauri ya mji wa Masasi nyumbani kwa mganga
huyo.
Alisema
wana familia hao walikumbwa na kadhia hiyo baada ya kuitwa na mganga
huyo msichana mwenye umri wa miaka 17 (jina tunalihifadhi) kwa lengo la
kwenda kumalizia dawa hiyo ya kinga kwa wanafamilia hao kutokana na
watoto wao wawili kupewa matibabu na mganga huyo wiki mbili zilizopita.
Mkuu
wa kituo, alisema kwa mujibu wa maelezo aliyoyatoa mganga, alitoa dawa
hiyo kwa wanafamilia hao waitumie kwa kuoga na kupaka kwenye miili yao
na si vinginevyo.
Alijieleza
kwamba, baada ya kuwapa, aliingia ndani ya nyumba yake lakini
wanafamilia hao walidanganywa na jirani yao (aliyetajwa jina) kuwa ili
kinga hiyo iwe ya kudumu na muda mrefu, ni lazima waoge na wanywe maji
yake.
Kwa
upande wao, wauguzi wa zamu; Prisca Mirumba wa wodi namba moja “B” ya
wanaume na Sophia Erasto wa wodi namba sita ya wanawake, walisema
waliwapokea wagonjwa hao juzi usiku saa 2:30 wakiwa wamepoteza fahamu
huku baadhi yao wakitokwa na mapovu vinywani.
Ilielezwa,
walibaini watu hao walipewa kimiminika kinachosadikika kuwa ni sumu.
Walipewa matibabu ya awali ingawa hadi sasa kwa mujibu wa wauguzi hao,
hali za wanafamilia hao si ya kuridhisha.
Chanzo cha dawa
Akizungumza kwa tabu akiwa amelazwa kwenye wodi namba sita Hospitali ya Mkomaindo mjini Masasi, baba wa familia hiyo, Geofrey Evance alisema chanzo cha yeye na familia yake kwenda kwa mganga huyo kupata tiba ni baada ya watoto wake kukumbwa na ugonjwa wa degedege.
Akizungumza kwa tabu akiwa amelazwa kwenye wodi namba sita Hospitali ya Mkomaindo mjini Masasi, baba wa familia hiyo, Geofrey Evance alisema chanzo cha yeye na familia yake kwenda kwa mganga huyo kupata tiba ni baada ya watoto wake kukumbwa na ugonjwa wa degedege.
Alisema
baada ya kufika kwa mganga, walipewa dawa hiyo ya nyungu na kisha
kushawishiwa na jirani yao wainywe dawa hiyo na kwamba mara baada ya
kunywa, walipoteza fahamu na walijikuta wakiwa hospitalini Mkomaindo,
mjini Masasi.
Social Plugin