|
Misaada mbalimbali kwa wahanga wa mvua ya Tonado iliyoambataba na upepo na mawe
yanayodaiwa kuwa na uzito wa kil0 20 imeendelea kutolewa kwa wahanga ambapo leo mkuu wa wilaya ya Nyang’wale mkoani Geita Ibrahim Marwa akiwa ameambatana na viongozi wa halmashauri hiyo amekabidhi msaada wa vyakula mbalimbali ikiwemo magunia 37 ya mahindi,unga wa
sembe kilo 180,mchele kilo 70,mafuta ya kula lita 74,chumvi kilo 110,dagaa debe
moja-picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog
Kushoto ni mkuu wa wilaya ya Geita ya Nyang’wale mkoani Geita Ibrahim Marwa akizungumza wakati wa kukabidhi msaada wa chakula na vitu vingine kama vile madaftari,sabuni,mapanga
na furushi la nguo na viatu.
Halmashauri ya Nyang'wale ni ya kwanza kupeleka msaada kwa wahanga hao kati ya halmashauri zote nchini Tanzania
Mkuu wa wilaya ya Nyang’wale mkoani Geita Ibrahim Marwa( aliyevaa miwani) akikabidhi mfuko wa unga kwa mkuu wa wilaya ya Kahama Benson Mpesya anayepokea misaada mbalimbali kutoka watu mbalimbali kwa niaba ya serikalli na wahanga wa mvua ya upepo na Mwakata Kahama iliyonyesha mapema mwezi huu
|
|
Kushoto ni mkuu wa wilaya ya Kahama Benson Mpesya akiwashukuru viongozi mbalimbali wa halmashauri ya
wilaya ya Nyang’wale mkoani Geita waliokuwa wameambatana na mkuu wa wilaya hiyo Ibrahim Marwa.Mpesya alisema halmashauri hiyo kutoka nje ya mkoa wa Shinyanga imekuwa mfano mzuri kwa kuona umuhimu wa kusaidia wahanga wa mvua ya Tonado |
|
Mkuu wa wilaya ya Nyang’wale mkoani Geita akipeana mkono na mkuu wa wilaya ya Kahama Benson Mpesya |
|
Mkuu wa wilaya ya Nyang’wale mkoani Geita akipeana mkono na mkuu wa wilaya ya Kahama Benson Mpesya baada ya kumaliza zoezi la kukabidhiana misaada hiyo |
|
Viongozi kutoka halmashauri ya wilaya ya
Nyang’wale mkoani Geita wakiwa katika picha ya pamoja na mkuu wa wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga-picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog |
Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com