Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

Aibu Kubwa!! MUME WA MTU ANASWA KWENYE KICHOCHORO AKIVUNJA AMRI YA 6 NA CHANGUDOA!!


Wakihamaki baada ya kukurupushwa.
Tukio hilo la aina yake lilinaswa kwenye uchochoro mmoja, maeneo ya Mwenge, Dar, majira ya saa 9:00 usiku ambapo wahusika hao ambao hawakutaka kutaja majina walikutwa wakiwa wanavunja amri ya sita kabla ya kushtuliwa na mwanga wa kamera za makachero wa OFM.
Wakiwa wanakatiza kwenye uchochoro huo, OFM walisikia miguno ya kimahaba ambapo ilibidi kutulia kidogo kujua kunani kinachoendelea mahali hapo.Waliposogelea waliwashuhudia wawili hao wakiwa wamevua nguo ambapo mwanamke alikuwa ametandika khanga chini bila kujali mtu anaweza kukatiza na kushuhudia sinema yao ya ngono.

Dada huyo akivaa baada ya fumanizi hilo.
Mara baada ya kuwafotoa picha kadhaa, wawili hao walishtuka huku mwanamke akivaa nguo harakaharaka kabla ya mwenzake naye kuvaa kisha wakataka kuanzisha timbwili kwa OFM.
 
Wakati wawili hao wakizozana na OFM kwa kosa la kuwakatishia ‘mambo’ yao, alitokea jamaa mmoja aliyekuwa akilinda jirani na eneo hilo hivyo kuwapa woga wawili hao.
Hata hivyo, OFM iliwatisha kuwa eneo hilo siyo gesti wala ndani hivyo walichokuwa wakikifanya siyo sahihi ndipo wakajikuta wakiomba yaishe bila kurushwa mtamboni.Kwa upande wake, mwanaume aliomba asamehewe akidai kuwa ni mume wa mtu na kama tukio hilo litaenda hewani itakuwa fedheha kwa familia yake.

“Huyu dada yeye hana shida sana kwani siyo mke wa mtu. Tatizo lipo upande wangu maana mkinitoa itakuwa fedheha kwa mke na watoto wangu,” alijitetea jamaa huyo bila kujua OFM walishakula kiapo cha kutokomeza uovu kwenye jamii.Baada ya aibu hiyo, wawili hao waliondoka mahali hapo na kutimkia kusikojulikana.
Chanzo-GPL

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com