|
Nyumba ikiwa imezingirwa maji huko Lamadi ambapo zaidi
ya wakazi 300 wa kijiji cha Lamadi
Wilayani Busega mkoani Simiyu hawana sehemu za kuishi kutokana na nyumba zao
kusombwa na maji kufuatia mvua kubwa iliyoambatana na upepo mkali kunyesha jana-Picha na Faustine Fabian Malunde1 blog- Simiyu
Nyumba zikiwa zimezingirwa maji
Hali ni mbaya |
|
Nyumba iliyoezekwa kwa nyasi ikiwa imebomolewa na mvua
|
Nyumba ya kienyeji ikiwa imezingirwa maji huko Lamadi Simiyu
eneo la tukio
*****
Zaidi
ya wakazi 300 wa kijiji cha Lamadi
Wilayani Busega mkoani Simiyu hawana sehemu za kuishi kutokana na nyumba zao
kusombwa na maji kufuatia mvua kubwa iliyoambatana na upepo mkali kunyesha jana majira ya usiku.
Mvua
hiyo ilisababisha mafuriko makubwa
ambayo yaliyosababisha nyumba zao kuingiliwa na maji na nyingine
kuezuliwa na upepo mkali.
Baadhi ya wakazi wa kijiji hicho wamehifadhiwa na ndugu na jamaa zao huku
wengine wakikimbilia katika taasisi
za serikali ikiwemo shule ya msingi Nyamajeshi iliyopo kijijini hapo kwa ajili ya usalama wa maisha yao.
Akizungumza katika eneo la tukio diwani wa kata ya
Lamadi Emanuel Desera alisema tukio hilo limetokea baada ya mvua hiyo kunyesha kwa muda mrefu hali iliyosababisha maji yazidi kujaa
katika maeneo ya wakazi ya watu na kusababisha nyumba nyingi kubomoka.
Desera alisema baada ya mvua hiyo kufanya uharibifu huo wananchi
hao walilazimika kukimbilia katika maeneo yaliyo salama ambapo ni shule ya
msingi Nyamajashi ili kunusuru maisha yao kutokana na nyumba zao kujaa
maji.
Alibainisha kuwa hali ya wananchi hao kwa hivi
sasa siyo nzuri kwani wahanga wengine
wamekimbilia kwa ndugu zao kujihifadhi, huku akibainisha kuwa mafuriko bado
yanaongezeka na kuiomba serikali kupeleka msaada wa chakula madawa na
mahema kwa wahanga hao.
“Vitongoji vilivyokumbwa na mafuriko hayo ni Kisesa,Sokoni Mwalukonge,Lukungu,Iseni B na Mwabayanda ambapo nyumba 200 zimesombwa na maji na watu zaidi ya 300 wapo
katika shule ya msingi Nyamajashi ili kuweza kujinusuru na mvua”,alisema Desera.
Mmoja wa wakazi wa jiji cha Lamadi Joseph Chenga ameiomba serikali kupitia ofisi
ya waziri mkuu kupeleka misaada ya mahema na chakula ili kuwawezesha wananchi
hao kupata chakula kwani mpaka sasa chakula walichokuwa wakikitegemea
kimesombwa na maji katika makazi yao.
Baadhi
ya wananchi hao wakiongea na waandishi wa habari waliofika katika tukio
hilo walisema kuwa maji hayo yamejaa kutokana na vijiji hivyo kuwa
kwenye bonde hali
ambayo mvua zikizidi maji hutuama na kukosa sehemu ya kuelekea hivyo
yanarudi katika makazi
ya watu.
”Mvua hiyo ilianza kunyesha majira ya saa sita
usiku ambapo maji yalijaa katika nyumba na kusomba vitu mbalimbali pamoja na
kuku hali iliyotulazimu kukimbilia katika katika shule ya msingi Nyamajashi kwa
ajili ya kujihifadhi,pamoja na kupata msaada zaidi kutoka serikalini”,alisema
mmoja wa waathirika wa mafuriko.
Viongozi
mbalimbali wakiwemo kamati ya ulinzi na
usalama ya wilaya hiyo ikiongozwa na mkuu wa polisi wa wilaya walifika
eneo la tukio na kujionea uharibifu huo ikiwa pamoja na kuangalia
usalama
wa wananchi hao waliokumbwa na mafuriko hayo.
|
|
Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com