ANGALIA PICHA_ WACHEZAJI WA SIMBA SC WATOA MSAADA KWA WATOTO WENYE ULEMAVU KITUO CHA BUHANGIJA MJINI SHINYANGA
Friday, April 03, 2015
Timu ya Simba Sc leo jioni imeweka historia mjini Shinyanga baada
ya kuwatembelea watoto wenye ulemavu wa ngozi(Albino),wasiosikia na wasioona
katika kituo cha Buhangija Jumuishi chenye watoto zaidi ya 370.Pichani ni
Msemaji
wa Simba SC, Hajji Manara baada
ya kushuka kwenye basi la Simba sc nje ya kituo cha kulelea watoto wenye
ulemavu cha Buhangija mjini Shinyanga-picha zote na Kadama Malunde-Shinyanga
Wachezaji wa timu hiyo wakiongozwa na Msemaji
wa Simba SC, Hajji Manara na kocha wa timu
hiyo Goran Kopunovic na wametoa msaada wa maji na juisi
na shilingi milioni moja kwa ajili ya kusaidia kituo hicho ikiwa ni siku moja
kabla ya mchezo wao na timu ya Kagera Sugar kwenye ligi kuu Vodacom Tanzania
bara utakaofanyika siku ya Jumamosi .
Wachezaji
wa Simba SC wakiingia kwenye kituo cha Buhangija mjini Shinyanga.
Simba SC inakuwa klabu ya kwanza nchini Tanzania kuwafikia
watoto wenye ulemavu ambapo katika kituo hicho kuna watoto wenye ulemavu wa
ngozi mpaka leo Ijumaa wapo 270.
Wachezaji wa Simba Sc wakipiga stori na watoto wenye ulemavu
wa ngozi .
Wachezaji wakiwa wamebeba watoto wenye ulemavu wa ngozi
Kushoto ni Msemaji
wa Simba SC, Hajji Manara akitafakari jambo
Mchezaji wa Simba SC akionesha bango
Mkuu
wa kituo cha Buhangija Jumuishi Peter Ajali akiwakaribisha wachezaji wa Simba
sc ambapo alisema hiyo ni klabu ya kwanza ya mpira nchini Tanzania kufika katika kituo
hicho.
Eneo la tukio
Watoto wenye ulemavu wa ngozi wakiwa kituo
Kocha wa timu Simba sc Goran Kopunovic akizungumza jambo katika kituo hicho
Wachezaji
wa Simba SC wakiwa wamebeba bango katika kituo cha Buhangija leo
Eneo la tukio
Wachezaji wa Simba sc wakiwa Buhangija
Mkuu
wa kituo cha Buhangija Jumuishi Peter Ajali akiwa na mchezaji wa Simba sc
wakiwa wameshikilia bango likisomeka “Imetosha mauaji ya Albino” ikiwa ni kauli
mbiu ya timu juu ya mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi yanaoendelea nchini
Tanzania.
Wachezaji wa Simba sc wakiwa Buhangija mjini Shinyanga
Mchezaji
wa Simba SC Ibrahimu Twaha akizungumza kwa niaba ya wachezaji wenzake ambapo
alieleza kusikitishwa na vitendo vya mauaji ya albino na kujikuta akitoa
machozi.
Kushoto ni Msemaji
wa Simba SC, Hajji Manara akiwa amebeba mtoto mwenye ulemavu wa ngozi ambapo aliwataka watoto hao kutokata tamaa kwani wapo watu wenye ulemavu wa ngozi kama yeye wamefanikiwa katika maisha
Mchezaji wa Simba sc Emmanuel Okwi akipiga stori na watoto wenye ulemavu wa ngozi
Watoto wenye ulemavu wa ngozi wakiwa wamebeba bango
Zoezi la kugawa juisi likiendelea
Kocha wa timu Simba sc Goran Kopunovic katika pozi na mtoto mwenye ulemavu wa ngozi leo
Wachezaji wa Simba sc wakiondoka kwenye kituo cha Buhangija-picha zote na Kadama Malunde-Shinyanga
Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Social Plugin