ANGALIA PICHA ZA AJALI MBAYA YA BASI NA LORI ILIYOUA WATU 18 LEO HUKO MOROGORO
Sunday, April 12, 2015
WATU 18 wamepoteza
maisha papo hapo kwa kuteketea na moto huku wengine 11 wakijeruhiwa
vibaya baada ya Basi la kampuni ya Nganga kugongana uso kwa uso na gari
la mizigo aina ya Mistubishi Fuso mkoani Morogoro.
Ajali hiyo imetokea leo
majira ya saa mbili asubuhi katika Kijiji cha Msimba, tarafa ya Mikumi,
Wilayani Kilosa mkoani Morogoro ikilihusisha basi hilo lenye namba T373
DAH na Fuso hilo lenye namba T164 BKG.
Kamanda wa Polisi mkoani
Morogoro Leonald Paulo amesema chanzo cha ajali hiyo ni dereva wa Basi
la Nganga kuendesha gari kwa mwendo kasi na kulipita gari lillilo mbele
yake bila kuchukua tahadhari na kusababisha ajali hiyo.
Amesema basi hilo
lililokuwa likitoka Dar-es-salaam kwenda Mbeya lilikuwa limepakia
pikipiki katika buti, ambayo ilikuwa na mafuta hivyo baada ya kugongana
palitokea mlipuko na kusababisha moto mkubwa ulioteketeza basi na lori
hilo.
Kamanda Paulo amesema
waliokufa ni madereva wa magari yote mawili walioteketea kabisa na moto
huo na abiria walioshindwa kujiokoa, na majeruhi takribani 11
wamekimbizwa katika Hospitali ya Mtakatifu Kizzito Mikumi.
Habari kwa hisani ya Father Kidevu Blog
Moto ukiteketeza magari hayo
Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Social Plugin