Mahakama ya Hakimu Mkazi wilaya ya Shinyanga imemhukumu kifungo cha maisha jela mkazi wa mtaa wa Kitangili katika manispaa ya Shinyanga baada ya kupatikana na hatia ya kumbaka na kumpa ujauzito mtoto wake wa kambo, mwanafunzi wa darasa la tatu.
Alimbaka mtoto huyo kutimiza masharti ya mganga ili kutoa tiba kwa mkewe.
Akisoma
hukumu hiyo jana, Hakimu Mkazi mwandamizi wa wilaya, Thomson Mtani
alisema mahakama imeridhika na ushahidi uliotolewa na upande wa
mashitaka ukiongozwa na wakili wa serikali, Judith Tuka.
Mtuhumiwa
Osward Charles (45) mkazi wa Kitangili alifikishwa mahakamani kwa
tuhuma mbili. Kosa la kwanza likiwa ni kumbaka mtoto wake mwenye umri
chini ya miaka kumi ambaye ni mwanafunzi kinyume na kifungu namba 130,
kifungu kidogo cha kwanza na cha pili na kifungu namba 131 kifungu
kidogo cha pili cha sura ya 16 cha kanuni ya adhabu.
Kosa
la pili ni kumwingilia kimwili mtoto wake ambaye ni mwanafunzi wa shule
na kumpa ujauzito kinyume na kanuni ya tano ya sheria ya elimu ya mwaka
2003 inayotoa adhabu kwa watu wanaowaoa na kuwapa mimba wanafunzi wa
shule kama ilivyo katika kifungu cha 35 kifungu kidogo cha tatu cha
sheria ya elimu ya 353.
Ilidaiwa
na mwendesha mashtaka mwanasheria wa serikali Judith Tukakuwa, kati ya
Novemba 12 mwaka 2012 na Septemba katika eneo la mtaa wa Kitangili
manispaa ya Shinyanga mshitakiwa alimbaka mtoto wake wa kambo ambaye ni
mwanafunzi mwenye umri wa miaka tisa na kumsababishia ujauzito.
Awali
mshitakiwa katika mwenendo wa kesi alikana kutenda makosa hayo lakini
katika utetezi wake mbele ya mahakama kabla ya kutolewa kwa hukumu hiyo
ili mahakama impunguzie adhabu alikiri kumbaka mtoto wake mbele ya mama
yake mzazi kwenye kitanda kimoja baada ya kupewa maagizo ya mganga wa
jadi kama sehemu ya tiba ya mke wake aliyekuwa akisumbuliwa na maradhi.
Social Plugin