Watangazaji Veronica Natalis,Richard Ndariro,DJ Hunter na msanii wa bongo movie Shinyanga aliyefukuzwa uanachama Amina Francis Mwandu |
Richard Ndariro,Kadama Malunde,Veronica Natalis na Amina Mwandu |
Kumekuwepo na sintofahamu baina ya wasanii katika kundi la wasanii wa kuigiza “Bongo Movie Shinyanga”,ambapo
baadhi ya wasanii wa kundi hilo wakimtupia lawama mwenyekiti wa Bongo Movie
Shinyanga.
Inaelezwa kuwa kinachoendelea hivi sasa ni kwamba mwenyekiti wa Bongo Movie Shinyanga Juma Ibrahimu
Songoro "Songoro Gaddafi" anashikiliwa na jeshi la polisi Shinyanga kwa kosa la kumtishia
kumuua aliyekuwa katibu wa Bongo Movie Shinyanga Sophia Kichochi baada ya kudai mshahara wake kutokana na kufanya kazi kwa muda mrefu bila kulipwa.
Miongoni mwa wasanii wa kundi hilo Amina Francis Mwandu anasema
migogoro imeanza mwezi Machi mwaka huu baada ya Filamu ya Firigisi kumaliza
kurekodiwa ambapo mwenyekiti alimfukuza katibu wake akidai kuwa anavujisha siri
za ofisi baada ya hapo akamfukuza pia msanii Amina Mwandu,mhusika mkuu katika filamu ya Firigisi inayohusu mauaji ya albino ambayo hata sokoni bado haijaingia.
Katika maelezo yake Songoro anasema alimfukuza katibu wake kutokana na utovu wa nidhamu huku akikanusha kuwa siyo katibu wake bali alikuwa mfagiaji tu katika ofisi yao.
Hapa nimekurekodia Interview iliyofanyika kwenye Kipindi cha
Faraja Mamboleo kinachorushwa na Radio Faraja fm ya Shinyanga kila siku Jumatatu
hadi Ijumaa kuanzia saa tatu asubuhi hadi saa saba mchana.
Utasikia sauti ya watangazaji Veronica Natalis(V2),Richard Ndariro (RND),DJ Hunter,msanii Dennis Sweya (Dino) wa Bongo Movie Dar es salaam director wa filamu ya Firigisi,Songoro,waandishi wa
habari Kadama Malunde na Chibura Makorongo.
Sikiliza/Download hapa chini ,chagua njia moja kati ya hizi 2
BOFYA HAPA KUSOMA HABARI YA KWANZA KUCHAPISHWA NA MTANDAO HUU KUHUSU BONGO MOVIE SHINYANGA