Mara
nyingi stori za aina hii huanza kusambaa kwenye mitandao ya kijamii,
baadae unaona RADIO na TV nazo zinaanza kuripoti.. Siku ya leo APRIL 9
watu walianza kusambaziana picha za ajali iliyotokea Tanga, mabasi
mawili ya abiria na gari dogo yamegongana, watu 10 wamefariki na wengine
kujeruhiwa.. kabla siku haijaisha naipokea hii nyingine kutoka
Morogoro.
Basi la Kampuni ya Happy Nation lenye namba T 618 BDN lililokuwa likitokea Dar es Salaam
kuelekea Mbeya limepata ajali na kutumbukia kwenye mfereji katika eneo la Mikumi mkoani Morogoro. taarifa
za awali zinasema watu wawili wamefariki na wengine kujeruhiwa.
Chanzo cha ajali hakijafahamika, naifuatilia hii kwa ukaribu.. kitakachonifikia nitakusogezea hapa muda wowote mtu wangu.
TAARIFA KAMILI TUTAWALETEA ......Endelea Kutembelea Malunde1 Blog
Social Plugin