Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

BASI LAGONGA MTU MWENYE UGONJWA WA AKILI,LAPINDUKA,LAUA HUKO PWANI


Taarifa zilizotufikia hivi punde kutoka chanzo cha kuaminika,zinaeleza kuwa Basi la kampuni ya GAMET Trans linalofanya safari zake Dar-Lindi-Masasi-Nachingwea limepata ajali maeneo ya Kibiti wilaya ya Rufiji-Utete mkoa wa Pwani .

Ajali hiyo imetokea baada ya dereva wa basi kutaka kumkwepa mtu anayedaiwa kuwa na tatizo la ulemavu wa akili,lakini kwa bahati mbaya likamgonga na kufariki papo hapo,taarifa zaidi zinaeleza kuwa baada ya ajali hiyo basi hilo liliacha njia na kupinduka na kupelekea kifo cha mtu mmoja aliyegongwa na wengine waliokuwemo ndani ya basi hilo  ambao idadi yao haikujulikana mara moja wamejeruhiwa.


Via>>Kibonajoro.com




Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com