BASI LAGONGA MTU MWENYE UGONJWA WA AKILI,LAPINDUKA,LAUA HUKO PWANI
Tuesday, April 14, 2015
Taarifa
zilizotufikia hivi punde kutoka chanzo cha kuaminika,zinaeleza kuwa
Basi la kampuni ya GAMET Trans linalofanya safari zake
Dar-Lindi-Masasi-Nachingwea limepata ajali maeneo ya Kibiti wilaya ya
Rufiji-Utete mkoa wa Pwani . Ajali hiyo imetokea baada ya dereva wa basi kutaka kumkwepa mtu anayedaiwa kuwa
na tatizo la ulemavu wa akili,lakini kwa bahati mbaya likamgonga na
kufariki papo hapo,taarifa zaidi zinaeleza kuwa baada ya ajali hiyo basi
hilo liliacha njia na kupinduka na kupelekea kifo cha mtu mmoja
aliyegongwa na wengine waliokuwemo ndani ya basi hilo ambao idadi yao haikujulikana mara moja wamejeruhiwa.
Via>>Kibonajoro.com
Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Social Plugin