Ajali ya uso kwa uso kati ya basi na
lori nchini Morocco imewaua watu 31 wengi wao wakiwa wanariadha vijana
,kulingana na maafisa.
Wanariadha tisa wameripotiwa kujeruhiwa karibu na mji wa kusini wa Tan-Tan.
Wengi wa waathiriwa wamefariki baada ya moto kulichoma basi hilo wakati wa ajali,kulingana na vyombo vya habari vya eneo hilo.
Ajali hiyo inadaiwa kutokea katika barabara kati ya mji mkuu wa Rabat na Laayoune ambao uko magharibi mwa Sahara.
Ilitokea
mapema siku ya Ijumaa katika wilaya ya mashambani ya Chbika karibu na
Tan -Tan kulingana na vyombo vya habari vya eneo hilo.
Wengi wa
wale waliokuwa wakisafiri basi hilo walikuwa wanafunzi waliokuwa
wakishiriki katika mashindano ya michezo kulingana na mtandao wa
le360.ma
Via>>BBC
Social Plugin