Habari tulizozipata hivi punde zinadai kuwa mashabaki Timu ya Simba SC wamefariki dunia na wengine zaidi ya 10 kujeruhiwa baada ya basi lao kupinduka eneo la Makunganya barabara ya Morogoro-Dodoma wakati wakielekea mkoani Shinyanga kushuhudia mchezo wa Ligi kuu Vodacom Bara kati ya Kagera Sugar vs Simba SC katika uwanja wa CCM Kambarage mjini Shinyanga unaotarajiwa kufanyika kesho Jumamosi.
Chanzo cha ajali hiyo kinadaiwa kuwa ni utelezi uliomfanya dereva wa gari hilo kushindwa kulimudu na kuserereka kabla ya kugionga ukingo wa barabara na kupinduka.
Taarifa zaidi kutoka eneo la tukio hilo zinasema majeruhi wamekimbizwa katika hospitali ya mkoa wa Morogoro kwa ajili ya matibabu.
Social Plugin