Huwa
inatokea Mwanaume anataka kumuoa mrembo flani lakini wazazi wa Mke
mtarajiwa wanakataa mtoto wao kuolewa na jamaa labda kwa sababu za
kidini, kitabia au kitabaka.
Basi hii imetokea Pakistani ambako Gul
Ahmed Said amemuua Baba Mkwe mtarajiwa pamoja na watu wengine tisa wa
familia yake baada ya kukataliwa kumuoa Binti wa Mzee huyo huko
Charsadda.
Charsadda |
Binti aliyekua anataka kumuoa ni binamu yake
ambapo Polisi wa Pakistani wamesema ugomvi ulianzia kwenye mabishano ya
idadi ya dhahabu kwenye harusi.
Waliouawa kwa risasi ni Watoto nane wa
mzee huyo, mzee mwenyewe pamoja na mke wake ambapo Polisi bado
wanaendelea kumtafuta Said ambaye amekua akitafutwa kutokana na mauaji
mengine aliyoyafanya November 2014 kwa kuwaua Wazazi wake, kaka yake
pamoja na shemeji yake.
Social Plugin