Mchezo wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara kati ya
wenyeji Kagera Sugar dhidi ya wapinzani wao Simba sc leo umeshindwa kufanyika
katika uwanja wa CCM Kambarage mjini Shinyanga kutokana na hali ya hewa kuwa
mbaya.
Kufuatia mchezo huo kushindwa kufanyika ilizuka tafrani kubwa
katika uwanja wa Kambarage iliyodumu zaidi ya masaa mawili ambapo viongozi wa
Simba na mashabiki wa soka mkoani humo wakitoa lawama kwa uongozi wa chama cha mpira mkoa wa Shinyanga SHIREFA chini ya mwenyekiti wake Benister
Lugola kuchangia mchezo huo kuahirishwa.
Akizungumza na malunde1 blog mkuu wa idara ya habari
na mawasiliano wa klabu ya Simba SCHaji Manara amesema kushindwa kufanyika kwa
mchezo huo ni njama ya uongozi wa mpira kwani hali ya uwanja ni nzuri na
inawezekana mchezo kuchezwa.
“Sisi kama Simba tunaamini kabisa kuwa uongozi wa FA
mkoa wa shinyanga hauja fanya vema kuzuia mchezo huu kwani wao wanacholenga ni
maslahi ya watu kuwa wachache uwanjani bila kujua sisi tunatumia gharama kukaa
hoteli kusubiri mchezo mwingine”alisema Manara.
Naye kocha msaidizi wa timu ya Kagera Sugar Mlange Kambange amesema maamuzi ya chama cha mpira mkoa wa Shinyanga yaliyofanyika
kuahirisha mchezo sio mazuri kwani wachezaji na mashabiki walikuwa na morali
licha hali ya hewa kuwa mbaya .
“Chama kimeamua vibaya kuahirisha mchezo kwani sisi
kama timu zote mbili tulikuwa tumekwisha kubali kwamba tucheze maana uwanja hauna
maji japo sehemu za magoli kuna maji kidogo”,alisema Kabange.
Kwa upande wake katibu wa chama cha mpira mkoa wa Shinyanga Said Nasoro amesema hali ya hewa ilikuwa hairusu mchezo huo kuchezwa
kutokana na hali ya hewa kuwa mbaya kwani uwanja umejaa maji baadhi ya maeneo
hivyo ungeathiri mchezo huo.
Mchezo huo sasa utapigwa siku ya tarehe 6 Jumatatu
hapo katika dimba la Kambarage huku kesho Stand United ya mjini Shinyanga itashuka
dimbani kucheza na Mtibwa Sugar katika michuano hiyo ya lig kuu ya Vodacom Tanzania
bara katika uwanja huo wa CCM Kambarage.
Na Philipo Chimi-Shinyanga