TAZAMA PICHA_FURUSHI LA NGUO LALETA KIZAA ZAA MJINI SHINYANGA
Thursday, April 09, 2015
Furushi likiwa karibu na barabara kwenye fensi ya minyaa mjini Shinyanga.
Kumetokea taharuki ya aina yake leo mchana mjini Shinyanga
baada ya Furushi lisilojulikana mmiliki wake kukutwa kwenye fensi ya shule ya
msingi Mwenge karibu na kanisa kubwa la KKKT mjini Shinyanga.Furushi hilo
likiwa limefungwa kwa umaridadi mkubwa lilikuwa limetelekezwa na mtu
asiyefahamika na kusababisha taharuki kubwa huku wengine wakihisi pengine kuna
mtoto mchanga katelekezwa,ama kuna silaha na mawazo mengine kadha wa kadha hali
iliyosababisha umati wa watu kufurika eneo hilo ili kujionea-Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog
Kufuatia taharuki hiyo askari polisi walifika na kuwaruhusu wananchi waliokuwa eneo hilo kufungua furushi hilo ili kujua ndani kulikuwa na nini(pichani zoezi la kufungua furushi likiendelea)
Baada ya furushi hilo kufunguliwa vitu vingi vilikutwa kama vile,nguo nyingi za ndani(sidiria na chupi),suruali za kike,dawa za kienyeji,mafuta ya kujipaka,vyombo,karatasi,picha za mama na mtoto ,madaftari,kadi za kliniki n.k Askari polisi akiwa ameshikilia (daftari)Counter Book lililokuwa kwenye furushi hilo linaloonekana kuwa ni la mwanafunzi. Miongoni mwa picha za mtoto iliyokutwa kwenye furushi hilo Picha ya binti/mama iliyokutwa kwenye furushi
Wakazi wa Shinyanga wakiwa eneo la tukio kushuhudia furushi hilo
Wakazi wa Shinyanga wakiwa eneo la tukio
Wananchi wakiangalia vitu vilivyokuwa kwenye furushi hilo
Baada ya kubaini kuwa hapakuwa na kitu kibaya kwenye furushi hilo,wananchi walitawanyika,askari polisi wakaondoka na furushi hilo baada ya kuomba wananchi wasaidie kubeba vitu hivyo
Askari polisi akisaidiana na wananchi kuchukua vitu hivyo kwa ajili ya uchunguzi zaidi
Muendesha baiskeli maarufu Daladala mjini Shinyanga akibeba furushi hilo na kulipeleka kwenye kituo cha polisi -Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog
Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Social Plugin