Basi mtu wako nikakutana na bonge la HEADLINE mtandaoni yaani.. “10 of the Coolest Homes in the World“, nikaingia faster nijionee PICHA za hizo nyumba kali huko DUNIANI.
Nilizokutana nazo kiukweli ilibidi nicheke,alafu nikaona sio vibaya na wewe mtu wanguvu uzione labda iko itakayokuvutia na wewe ukatamani siku moja uwe nayo.
Unaambiwa hii inaitwa Antilia, iko India. Nayo iko kwenye list mtu wangu.
Inaitwa Bio Climatic Solar House, iko Ufaransa. Ilivyokaa kaa ni kama siyo mjengo wa kuishi vile.
Boeing 727 House, hii sio mara ya kwanza kuiona mtu wangu. Haikunishtua nilipoiona tena.
Ilinipa tabu kujua nini kinaendelea hapa. Naona kama mapango mapango tu hivi, lakini ndiyo mjengo huo mtu wangu. Bubble House, iko Ufaransa.
Duuh, jina lake tu ni balaa . Inaitwa Crazy House, iko Vietnam.
Mjengo huu uko Ivory Coast, hivi kama kuna watu mjusi tu wanaogopa, itakuwa kulala kwenye huyu mamba? Nyumba hiyo, inaitwa Crocodile House.
Hii nayo ni ghorofa ya aina yake . Dar-al-Hajar, iko Yemen.
Buti la kijeshi??? Hapana, huo ni mjengo kabisa mtu kajitengenezea hapo, inaitwaShoe House, iko South Africa.
Hii ya Korea Kusini nayo iko kwenye list, inaitwa Toilet House, kwa juu ukiicheki ni kama choo kweli.
Hiyo Toilet House ya Korea inavyoonekana kwa juu.
Kama imepinduka hivi.. kumbe hapo ndiyo iko sawa. Hujaipenda hii mtu wangu? Wenyewe wanaiita The Upside Down House, iko Poland.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Social Plugin