Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

KUTANA NA NYUMBA HIZI 10 ZENYE MAUMBO YA AJABU SANA DUNIANI,NIMECHEKA SANA BAADA YA KUZIONA

Crocodile-House-Ivory-Coast


Basi mtu wako nikakutana na bonge la HEADLINE mtandaoni yaani.. “10 of the Coolest Homes in the World“, nikaingia faster nijionee PICHA za hizo nyumba kali huko DUNIANI.
Nilizokutana nazo kiukweli ilibidi nicheke,alafu nikaona sio vibaya na wewe mtu wanguvu uzione labda iko itakayokuvutia na wewe ukatamani siku moja uwe nayo.
Antilia-India
Unaambiwa hii inaitwa Antilia, iko India. Nayo iko kwenye list mtu wangu.
Bio-Climatic-Solar-House-France
Inaitwa Bio Climatic Solar House, iko Ufaransa. Ilivyokaa kaa ni kama siyo mjengo wa kuishi vile.
Boeing-727-House-Costa-Rica
Boeing 727 House, hii sio mara ya kwanza kuiona mtu wangu. Haikunishtua nilipoiona tena.
Bubble-House-France
Ilinipa tabu kujua nini kinaendelea hapa. Naona kama mapango mapango tu hivi, lakini ndiyo mjengo huo mtu wangu. Bubble House, iko Ufaransa.
Crazy-House-Vietnam
Duuh, jina lake tu ni balaa . Inaitwa Crazy House, iko Vietnam.
Crocodile-House-Ivory-Coast
Mjengo huu uko Ivory Coast, hivi kama kuna watu mjusi tu wanaogopa, itakuwa kulala kwenye huyu mamba? Nyumba hiyo, inaitwa Crocodile House.
Dar-al-Hajar-Yemen
Hii nayo ni ghorofa ya aina yake . Dar-al-Hajar, iko Yemen.
Shoe-House-South-Africa
Buti la kijeshi??? Hapana, huo ni mjengo kabisa mtu kajitengenezea hapo, inaitwaShoe House, iko South Africa.
The-Toilet-House-South-Korea
Hii ya Korea Kusini nayo iko kwenye list, inaitwa Toilet House, kwa juu ukiicheki ni kama choo kweli.
toilet
Hiyo Toilet House ya Korea inavyoonekana kwa juu.

.
Kama imepinduka hivi.. kumbe hapo ndiyo iko sawa. Hujaipenda hii mtu wangu? Wenyewe wanaiita The Upside Down House, iko Poland.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com