Idhaa yako ya kiswahili ya BBC imekuandalia ukurasa wa habari za moja kwa moja kufuatia shambulizi la chuo kikuu nchini Kenya.
19.24pm:
Serikali
ya Kenya imetuma ujumbe katika mtandao wake wa Twitter ikisema kuwa
Watu 500 wameokolewa huku 70 wakiuawa wakiwemo wapiganaji 4 wa kundi la
Alshabaab #OneKenya voa CS @InteriorKE"
19.08pm:Majeruhi:
Baadhi ya majeruhi ambao
walisafirishwa kwa njia ya ndege kutoka Garissa wamewasili ili kupata
matibabu katika hospitali kuu ya Kenyatta mjini Nairobi Kenya.
17.10pm:Rais wa Kenya:
Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya
ametuma risala za rambi rambi kwa familia za wale waliouawa katika
shambulizi la chuo kikuu cha Garissa kazkazini mashariki mwa
Kenya.
Kiongozi huyo vilevile amewahakikishia wakenya kwamba serikali yake imechukua hatua za kuwapeleka maafisa wa usalama katika eneo hilo.
Amewataka wakenya kuwa watulivu wakatu huu ambapo maafisa wa usalama wanakabiliana na wapiganaji hao.
Kiongozi huyo vilevile amewahakikishia wakenya kwamba serikali yake imechukua hatua za kuwapeleka maafisa wa usalama katika eneo hilo.
Amewataka wakenya kuwa watulivu wakatu huu ambapo maafisa wa usalama wanakabiliana na wapiganaji hao.
17.00pm:Waziri wa usalama Kenya:
Waziri
wa maswala ya ndani nchini Kenya Joseph Nkaiserry amethibitisha kuwa
watu 15 wameuawa huku wengine 53 wakijeruhiwa kufuatia shambulizi la
alfajiri katika chuo kikuu cha Garissa nchini Kenya.miongoni mwa
waliofariki ni walinzi wawili wa mlango wa chuo hicho.
Akizungumza kutoka Garissa Nkaiserry amesema kuwa oparesheni ya kuwasaka wahalifu hao itaendelea hadi mateka wote waokolewe.
Akizungumza kutoka Garissa Nkaiserry amesema kuwa oparesheni ya kuwasaka wahalifu hao itaendelea hadi mateka wote waokolewe.
16.50pm:Mshukiwa mkuu:
Serikali
ya Kenya imemtaja Mohammed Kuno kama mshukiwa mkuu aliyepanga njama za
shambulizi la chuo kikuu mjini Garissa.Katika taarifa kwa vyombo vya
habari waziri wa usalama nchini Kenya Joseph Nkaiserry alitoa zawadi ya
dola 53,000 kwa mtu yeyote atakayemkamata mshukiwa huyo ama kutoa habari
zake.Kuno anajulikana kama 'Gama'adhere kwa jina maarufu.
15.10pm:Mitandaoni:
Mwandishi wa habari wa Kenya
Dennis Okari ambaye yuko katika eneo la chuo kikuu cha Garissa ameandika
katika mtandao wake wa Twitter akisema kuwa:Wapiganaji hao wako katika
jumba la kulala wanafunzi .''ninaweza kusikia milio ya risasi kutoka
upande wa pili.@ntvkenya".
14.48pm:Mahitaji ya Damu:
Kufuatia shambulizi la chuo
kikuu cha Garissa ,Shirika la msalaba mwekundu Red Cross limewataka raia
wa Garissa kutoa msaada wa damu.Walioitikia wito huo tayari wameeleka
katika hospitali kuu ya Garissa mbapo kituo cha kutoa damu kilianzishwa
chini ya mti.
14.40pm:Shahidi wa shambulizi:
Mwanafunzi
wa chuo kikuu cha Garissa Collins Wetangula amesema kuwa wakati
wapiganaji hao walipoingia katika nyumba anayolala aliwasikia wakifungua
milango na kuwauliza watu iwapo ni waislamu ama wakristo.''kama wewe ni
mkristo unapigwa risasi papo hapo.kila mlio wa risasi nilipousikia
nilidhani nitauawa'',aliambia shirika la habari la AP.
Amesema kwamba maafisa wa usalama baadaye waliingia kupitia dirisha moja na kumtoa yeye na wenzake hadi katika eneo salama.
Amesema kwamba maafisa wa usalama baadaye waliingia kupitia dirisha moja na kumtoa yeye na wenzake hadi katika eneo salama.
14.30pm:
Maafisa wa matibabu kwa sasa wanaelekea katika hospitali ya kuu ya Garissa nchini Kenya ili kusaidia wale waliojeruhiwa
Maafisa wa matibabu kwa sasa wanaelekea katika hospitali ya kuu ya Garissa nchini Kenya ili kusaidia wale waliojeruhiwa
14.00pm:Kwa ufupi
Takriban watu 15 wanaodaiwa kufinika nyuso zao wameshambulia chuo kikuu cha Garrissa Kaskazini mashariki mwa Kenya.
Watu
hao wanaodaiwa kuingia katika taasisi hiyo mwendo wa saa kumi asubuhi
wakati ambapo waislamu walikuwa wakifanya sala yao ya alfajiri.
Hatahivyo maafisa wa polisi wanasema kuwa shambulizi hilo lilifanyika mwendo wa saa kumi na moja unusu.
Mwandishi wa BBC mjini humo
anasema kuwa walinzi wawili waliuawa katika lango la chuo hicho huku
maafisa wawili wa polisi waliokuwa wakilinda chuo hicho pamoja na
wanafunzi wakijeruhiwa.
Walioshuhudia wanasema kuwa kumekuwa na majeruhi mengi ndani ya chuo hicho.
Mwandishi wetu anasema kuwa wapiganaji hao bado wako ndani ya chuo hicho na wamewateka nyara watu kadhaa.
Jeshi la Kenya KDF ,maafisa wa
polisi na amabulansi wamefika katika eneo la tukio na sasa wameingia
ndani ya majengo ya chuo hicho ambapo kumekuwa na ufyatulianaji wa
risasi kati ya washambuliaji na maafisa wa jeshi.
13.40pm:Waislamu
na wakristo waliotekwa ndani ya Jumba hilo la Chuo kikuu cha garissa
wamedaiwa kutawanywa kabla ya waislamu 15 kuwachiliwa huru kulingana na
msemaji wa kundi hilo la Alshabaab.
13.35pm:Serikali ya kenya
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta anatarajiwa kulihutubia taifa kufuatia shambulizi hilo la chuo kikuu cha Garrisa mapema leo.
13.30pm:Alshabaab:
kundi la wapiganaji wa Alshabaab limesema kuwa liko ndani ya Chuo hicho kikuu na limewatawanya waislamu na wakristo.
13.20pm:Wapiganaji
wamedaiwa kuwateka nyara wanafunzi na kuwaua watu 14 katika chuo hicho
kulingana na wafanyikazi wa msaada na maafisa wa polisi.Takriban watu 65
wengine wamejeruhiwa baada ya washambuliaji kuvamia chuo hicho.Vituo
vya habari nchini kenya hatahivyo vinaiweka idadi hiyo kuwa watu 16.
13.05pm:Idadi ya watu waliouawa kufuatia shambulizi la wapiganaji wa kundi la alshabaab imefikia 14
13.03pm:Al shabaab
Kundi la wapiganaji wa
Al-shabaab limekiri kutekeleza shambulizi katika chuo kikuu cha Garissa
Kaskazini mashariki mwa Kenya huku likiwaua watu 14
12.47pm:Wanafunzi
Chuo hicho cha Garissa kina takriban wanafunzi 1000, na wafanyikazi wengine.
12.30pm Wanafunzi:
Baadhi ya wanafunzi wamedaiwa kutoroka kutoka mabweni waliokuwa wakilala
12.20pm:Wapiganaji
Wapiganaji hao wanaodaiwa kuwa watano wanaaminika kuwa ndani ya jengo hilo la Chuo kikuu .
12.18pm:Kenya Red Cross
Shirika la msalaba mwekundu
nchini Kenya linasema kuwa watu 30 wamejeruhiwa huku wanne kati yao
wakiwa na majeraha mabaya..Kwa sasa shirika hilo linawasafirisha
madaktari katika eneo hilo.
11.30am Idadi ya watu
waliouawa kufuatia shambulizi la chuo kikuu cha Garrissa Kaskazini
mashariki mwa Kenya imefikia watu sita huku wengine 29 wakidaiwa
kujeruhiwa.
CHANZO-BBC
CHANZO-BBC