Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

Hali Ni Mbaya!! NJAA KALI HUKO KISHAPU,WANANCHI WASHINDIA UJI KAMA WAGONJWA!!

Licha ya kuwepo kwa mabadiliko ya tabia nchi nchi na sasa mvua za
masika kuanza kunyesha maeneo mbalimbali mkoani Shinyanga ikiwemo
wilaya ya Kishapu hali ya chakula ni tete kwa wananchi wilayani Kishapu.


Hali ni mbaya kattika kata za Mwamalasa,Lagana,Masanga,Shagihili na
Mondo katika wilaya hiyo yenye jumla ya kaya 42,000 na watu
wanaokadiriwa kuwa zaidi ya 272,990 kwa mujibu wa sense ya mwaka
2012.

Akizungumza na Nyahore Blog, Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa
(MNEC)wa wilaya hiyo,Boniface Butondo jana alisema licha ya mvua
kuanza kunyesha lakini wananchi katika maeno hayo wanalazimika
kushindia uji kama mlo kamili kufuatia mazao yao kuathiriwa na jua
kali lililodumu takribani miezi mitatu sasa na kukausha mazao yao
ikiwemo mtama na mazao ya jamii ya mikunde.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com