Haya ni baadhi matairi ya magari yalichomwa na baadhi wananchi
maeneo ya stendi kuu ya Ubungo jijini Dar ila Polisi wametumia mabomu ya
machozi kuwatawanyisha wananchi hao. Lakini baadhi ya Wananchi
hawakukubali hilo nao wakaanza kushika mawe na kuwarushia Polisi, ikawa
ni mawe VS Mabomu. Haya yote chanzo ni mgomo wa Madereva ulioanza leo nchi nzima.
Wananchi wakitumia lori kusafiri |
Katika eneo la stendi ya Ubungo polisi imewalazimu kutumia mabomu ya
machozi kusambaratisha abiria waliokuwa wamekusanyika eneo hilo wakitaka
kujua hatma ya usafiri wao kwenda mikoani.
Kuna taarifa kuwa zaidi ya mabasi 10 kutoka mikoa ya kanda ya Ziwa yamekwama wilayani Kibaha wakihofia vurugu kutokana na mgomo unaoendelea.
Hii picha ni mabasi yaendayo mikoani yakiwa ndani ya stendi ya Ubungo yamegoma kufanya kazi yoyote
Umati wa watu eneo la Ubungo stendi, uliosababisha Polisi kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya
Umati wa watu eneo la Ubungo stendi, uliosababisha Polisi kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya
Hii picha ni mabasi yaendayo mikoani yakiwa ndani ya stendi ya Ubungo yamegoma kufanya kazi yoyote
Mabasi yaendayo mikoani yakiwa Stendi ya Ubungo yamepaki.
Wasafiri wakiwa hawajui hatma ya safari yao eneo la Ubungo.
Hali halisi ya Ubungo ilivyokuwa asubuhi leo.
Muonekano wa eneo la Ubungo-Darajani hali ilivyokuwa.
Kituo cha daladala cha Shekilango hali ilivyokuwa.
Umati
mkubwa wa watu ukimshudia jamaa mmoja aliyekuwa akitoa ibada fupi ya
kuombea nchi kuhusiana na mgomo wa madereva ambao ni wa nchi nzima eneo
la Ubungo.
Usafiri wa bodaboda ukionekana kufanya kazi bila kugoma.
Abiria wakitafakari kuhusu safari yao.
Mwandishi wetu amezunguka maeneo tofauti tofauti jijini Dar na kujionea hali halisi ya mgomo wa mabasi ya mikoani pamoja na daladala za maeneo tofauti ya Jiji la Dar.
Mwandishi wetu pia aliweza kufika eneo la Stendi ya Ubongo na kujionea hali ilivyokuwa asubuhi na kuzungumza na baadhi ya madereva ambao walikuwa na kauli tofautitofati kuhusiana na mgomo huo.
Mmoja wa madereva ambaye alijitambulisha kwa jina la Ally Abdallah Shalon anayefanya kazi zake kati ya Dar es Salaam na Dodoma, alisema kuwa sababu kubwa ya kutokufanya shughuli zake ni kutokana na kikao ambacho walipanga kukifanya leo kujadili agizo la Sumatra lililowataka waende shule kusoma.
Dereva mwingine aliyejitambulisha kwa jina moja la Khamis anayefanya shughuli zake kati ya Mwanza na Dar es Salaam alisema sababu iliyomfanya agome ni kupinga sheria mpya ya Sumatra iliyopitishwa na jeshi la polisi kuwataka madereva wote wa abiria (Pasangers Services Vehicle) kwenda kusoma kozi ya miezi miwili kwa gharama ya shilingi laki tano.
Khamis alisema sheria hiyo inawabana sana madereva kwani moja kati ya vipengele vya sheria hiyo imeeleza kuwa, dereva yeyote atakayekamatwa akiwa amezidisha mwendo kasi hakuna faini yoyote bali unapelekwa mahabusu kwa muda wa siku kumi na nne baada ya kumaliza siku hizo, anapelekwa mahakamani kujibu shitaka linalomkabili.
“Hii sheria inatubana sana, mtu ukihitaji kubadilisha leseni yako
ikipitwa na muda unatakiwa kurudia tena kwenda kusoma darasani kwa muda
wa wiki mbili kwa ada isiyopungua laki tano na kuendelea kitu ambacho
kinatuumiza sisi madereva,” alisema Khamisi
SOMA HABARI ZAIDI HAPA
Social Plugin