Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

HII HAPA ORODHA YA MAKOCHA 10 WA SOKA WANAOLIPWA MSHAHARA MKUBWA ZAIDI DUNIANI

List ya makocha wa mpira wa miguu wanaoongoza kwa kulipwa vizuri kwenye soka mpaka sasa ambapo namba 1 imechukuliwa na Pep kama unavyoona list nzima hapa chini
1. Pep Guardiola

Pep Guardiola, Bayern Munich manager
Huyu ni kocha wa Bayern Munich, ameitumikia timu yake kwa mafanikio makubwa huk akiisaidia kupata mataji mbalimbali, ndiye kocha anayeongoza kwa kulipwa mshahara mkubwa kuliko wote kwa kupokea kiasi cha dola milioni 24
2. Jose Maourinho
mor
Huyu ni kocha wa Chelsea ambaye anajulikana kwa kuwa na maneno mengi,kwa sasa yupo mbioni kuwania ubingwa wa ligi kuu ya England, ni kocha anashika nafasi ya pili kwa kulipwa kiasi kikubwa cha pesa na hupokea kiasi cha dola milioni 17.
3. Marcello Lippi
macelo
Ana mchango mkubwa kwenye Timu ya Taifa ya Italy na kufanikiwa kutwaa kombe la dunia mwaka 2006, anapokea kiasi cha dola milioni 14.
4. Fabio Capello
capelo
Huyu ni kocha wa timu ya Taifa ya Russia, anapokea kiasi cha dola milioni 13
5. Carlo Ancelotti
carlo
Huyu ni kocha mkuu wa Real Madrid, anapokea kiasi cha dola milioni 10.5.
6. Arsene Wenger
Arsene Wenger, Manager of Arsenal
Amekuwa kocha wa Arsenal toka mwaka 1996, na anapokea kiasi cha dola milioni 10.
7. Gerardo Martino
gera
Huyu ni kocha wa Argentina, anapokea kiasi cha dola milioni 7.5.
8. Jurgen Klopp
jurge
Huyu ni kocha wa Borrusia Dortmund, anapokea kiasi cha dola milioni 6.
9. Manuel Pellegrini
pele
Huyu ni kocha wa Manchester City, anapokea kiasi cha dola milioni 5.75.
10. Jorge Jesus
benfic
Huyu ni kocha wa klabu ya Benefica tangu mwaka 2009, anapokea kiasi cha dola milioni 5.5

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com