Kila siku watafiti wana habari mpya kuhusiana na maisha, tumeona tafiti nyingi zikifanywa zikiwemo za magari, majumba watu maarufu, zote zikiwa ni sehemu ya maisha yanayotuzunguka kila siku
Lakini sikuwahi kufikiri kwamba kuna siku nitakutana na utafiti unaozunngumzia urefu wa maraisi duniani.
Leo nakusogezea utafiti uliofanywa January 4, 2015 ambao unazungumzia marais 10 ambao ni warefu zaidi duniani:-
1. Filip Vujanovic
Papa Benedict xvi akiwa na Rais wa Montenegro ambaye ndiye rais mrefu kuliko wote duniani, ana urefu wa futi 6.5
2. Nicolas Maduro
Huyu ni Rais wa Venezuela, anashika nafasi ya pili kwa kuwa rais mrefu, ana urefu wa futi 6.3
3. Bashar Al- Assad
Huyu ndiye Rais wa nne kwa urefu duniani kutoka Syria, ana urefu wa futi 6.2
4. Stephen Harper
Huyu ni Waziri mkuu wa Canada, ana urefu wa futi 6.2
5. Toomas Hendrik Ilves
Huyu ni rais wa Estonia ambaye pia aliwahi kuwa mwandishi wa habari, ana urefu wa futi 6.2
6. Paul Kagame
Kwa Afrika huyu ndiye rais anayeongoza kwa urefu, lakini duniani anakamata nafasi ya sita kwa futi 6.2 huku binti yake akimzidi kwa kuwa na futi 6.6
7. Barack Obama
Barack Obama ni Rais wa Marekani, ana urefu wa futi 6.1 huku mke wake Michelle Obama akiwa na futi 5.11
8. David Cameroon
Huyu ni Waziri mkuu wa Uingereza, urefu wake haujatofautiana na wa Rais Obama wa Marekani, wote wana futi 6.1
9. Blaise Compaore
Huyu ni Rais wa Burkina Faso ambaye Oktoba mwaka jana aliamua kujiuzulu kutokana na machafuko nchini kwake, ana urefu wa futi 6
10. Recep Tayyip Erdogan
Huyu ni rais wa Uturuki aliyekabidhiwa madaraka mwaka jana, ana urefu wa futi 6
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Social Plugin