Jamaa ambaye jina halikuweza kupatikana mara moja, amejikuta akionja
joto ya jiwe baada ya kudaiwa kukutwa akiiba kwenye shamba la mahindi
hivyo kulazimishwa kula mahindi mabichi.Tukio hilo la aina yake lilijiri
hivi karibuni kwenye Kata ya Miembeni, Bukoba mkoani Kagera na kuibua
gumzo kubwa.
Kwa mujibu wa shuhuda wetu, baada ya kumnasa kijana huyo akiiba mahindi
aliyoyajaza kwenye gunia, wamiliki wa shamba hilo walimuamuru kukaa
chini na kuyala yakiwa mabichi hadi yaishe, kitendo ambacho jamaa huyo
alikubaliana nacho.
Ilielezwa kwamba, katika hali ya kushangaza, kijana huyo hakukataa wala
kuonesha kutetereka kwani alianza kuyala hadi alipoamriwa kuacha na
kuambiwa aondoke.Katika habari hiyo iliyoripotiwa na Mtandao wa
Harakati, kijana huyo alionekana kuwa na matatizo ya kutosikia vizuri
wala kuongea kwa maana ya kuwa ni ‘bubu’.
Hata hivyo, kijana huyo hakujulikana alitokea wapi kwani mbali na madai
ya wizi na ububu pia hakuonekana mwenye ufahamu mzuri kutokana na mavazi
aliyokuwa amevaa.
NA HAMIDA HASSAN
Social Plugin