Mtuhumiwa huyo wa
mauaji ya kushangaza ana umri wa miaka thelathini na mmoja jina lake ni
Henry Chau aliibua hisia za walio wengi katika kesi ya namna yake mnamo
2013 wakati kichwa cha mamake mkubwa pamoja na babake vilipobainika
kuhifadhiwa katika majokofu mawili tofauti.
Majaji wa mahakama kuu
nchini Hong Kong ,wakati kesi hiyo ilipokuwa ikiendelea walisikiliza
namna Chau alivyotekeleza mauaji yake ,kwanza Kuua, pili Kutawanya
viungo vya maiti na kisha huwanyunyizia chumvi ili kuongeza ladha.
Yeye anasema yote hayo ni matokeo ya mapenzi yake kwa nyama choma ya kiti
moto,na nyama hiyo ya binaadamu zikisha iva ama kuchomwa huwa anafunga
nyama hizo katika makasha ya chakula pamoja na ubwabwa.
Polisi
walipofanya upekuzi katika nyuma yake walikuta baadhi ya viungo katika
chombo cha kuhifadhia taka.
Akitoa hukumu dhidi ya kesi hiyo,jaji
Michael Stuart-Moore alimuelezea Chau kama mbinafsi mwenye msongo wa
mawazo kutokana na mafanikio mabaya yake ya maisha na asiye na huruma
kwa wengine.
Chau, alihukumiwa adhabu mara mbili kifungo cha
maisha jela na miaka tisa na miezi minne kwa makosa mawili tofauti kwa
kuvunja sheria ya kuzika miili ya familia yake isivyo kawaida kosa
ambalo alikiri baadaye.
Rafiki wa Chau anayehusishwa katika mauaji hayo alikutwa hana hatia mwishoni mwa wiki iliyopita .
Taarifa
za kupotea kwa wanafamilia wa Chau zilipoibuliwa ,Chau alidanganya kuwa
jamaa zake walikwenda China,lakini baadaye alijisahau na kumuandikia
rafikiye kupitia ujumbe mfupi wa simu kwamba aliwaua jamaa zake.
Chau
mwenyewe hujiita mwendawazimu katika ujumbe aliokuwa akiwatumia watu
wake wa karibu na kusema kwamba hawezi kumuonea huruma mtu yeyote
kutokana na maumivu aliyopitia wakati wa makuzi yake utotoni mpaka
anakuwa mtu mzima.
Na alimua kuwadanganya polisi ilia pate wasaa wa
kuwaaga marafiki zake.
Via>>BBC
Social Plugin