Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MAJAMBAZI YAUA MWANAJESHI HUKO IRINGA TANZANIA

 
Watu wawili wamefariki mkoani Iringa akiwemo askari wa Jeshi la kujenga Taita (JKT) na mtu mmoja anayetuhumiwa kuwa ni jambazi wakati wa kurushiana risasi na jeshi la polisi baada ya kufanya uporaji eneo la Mafinga wilaya ya Mufindi.

Kamanda wa Jeshi la polisi mkoa wa Iringa ACP Ramadhani Mungi amesema Salma Semwiko mfanyabiashara na mkazi wa Mafinga akiwa anaelekea kazini alivamiwa na mtu aliyekuwa na silaha aina ya SMG kisha kumpora simu na fedha zaidi ya laki saba.

Ameongeza kuwa baada ya uporaji huo ilitokea pikipiki aina ya bodaboda na kumchukua jambazi huyo kisha kukimbilia eneo la Kinyanambo na ndipo yalipotokea majibizano ya silaha wakati polisi na wananchi wakifanya jitihada za kuwakamata majambazi hao.

Kamanda Mungi amesema Saidi Ng’umbi askari wa JKT amefariki papo hapo baada ya kupigwa kifuani upande wa kulia na majambazi hao.
 
Amesema jeshi la polisi wamefanikiwa kumkamata jambazi mmoja ambaye amefariki wakati akiendelea kupatiwa matibabu baada ya kupigwa kwenye paja la mguu.

Aidha ameongeza kuwa jeshi la polisi mkoani Iringa linaendelea na uchunguzi zaidi wa tukio hilo ikiwa ni pamoja na kumtafuta jambazi aliyekimbia katika tukio hilo.

Wakati huo huo Kamanda Mungi amesema Winifrida Frank umri wa miaka 25 mkazi wa eneo la Ipogolo Manispaa na Mkoa wa Iringa anashikiliwa na jeshi la polisi kwa tuhuma ya mauaji ya kumtupa mtoto mwenye umri siku tatu kwenye shimo la maji machafu.
 
Na  Yonna Mgaya-Malunde1 blog Iringa

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com