Watu sita wamekamatwa na Polisi kwa tuhuma za kumbaka mwanamke mmoja mwenye umri wa miaka 40.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Kusini Unguja Juma Saad Khamis, alisema hilo ni moja ya matukio mabaya kuripotiwa kufanywa katika kipindi cha maadhimisho ya sikukuu ya Pasaka.
“Watu hao walikamatwa Jumapili saa 2 usiku wakihusishwa kuhusika na tukio hilo,” alisema.
Uchunguzi wa awali unaonesha kuwa siku ya tukio watuhumiwa walionekana wakinywa na mwanamke huyo na baadaye walianza kumpiga na kumchukua hadi maeneo ya Bwejuu.
Hata hivyo Kamanda Khamis alikataa kutoa maelezo ya kina kuhusiana na watuhumiwa hao kwa maelezo kuwa yanaweza kuvuruga upelelezi wa tukio hilo ambao unaendelea kufanywa na mamlaka husika.
Alisema ukiacha tukio hilo baya, wananchi walisherehekea kwa amani sikukuu ya Pasaka.
“Kulikuwa na amani, nawashukuru polisi wa doria kwa kazi yao nzuri na kusababisha wananchi kusherehekea sikukuu kwa amani,” alisema Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mjini Mkadam Khamis Mkadam.
Kamishna Msaidizi (ACP) Mkadam alisema kulikuwa na matukio madogo ya ajali za barabarani, naye Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Mohamed Msangi alisema katika mkoa wake hakukuwa na matukio mabaya
Social Plugin