Mwanamme mmoja kwenye mji wa
Colorado nchini Marekani huenda akachukuliwa hatua za kisheria kufuatia
kisa ambapo alikasirishwa na kompyuta yake kisha akaitoa nje na
kuifyatulia risasi mara nane.
Polisi wanasema kuwa Lucas Hinch
alikuwa na matatizo ya kiteknolojia ndipo akaipeleka kompyuta hiyo upande
wa nyuma ya nyumba yake na kuiharibu ambapo alikamatwa muda mfupi
baadaye.
Vyombo vya habari vilisema kuwa alichoka na kusumbuliwa
na kompyuta yake lakini hakufahamu kuwa alikuwa akivunja sheria
alipoiadhibu kwa risasi.
Gazeti moja lilisema kuwa wakati herufi
za ctrl+alt+delete zilifeli , bwana Hinch alishikwa na hasira nna kuamua
kulipiza kisasi kwa kuiharibu Kompyuta hiyo hadi kiwango ambacho
haiwezi kutumika tena
Social Plugin