Maajabu!
Msichana aliyefahamika kwa jina la Dora mkazi wa Magomeni Bagamoyo
mkoani Pwani, hivi karibuni amejikuta akijifungua nazi badala ya mtoto,
jambo lililomshangaza kila mtu.
Ushirikina watajwa,
Ushirikina watajwa,
Ilidaiwa
kuwa, chanzo cha Dora kujifungua nazi ni maneno aliyoambiwa na mke
mwenzake aliyefahamika kwa jina la Jamila ambapo aliambiwa hatajifungua
kiumbe cha kawaida na ndipo alipokimbilia Dodoma kukwepa matatizo.
Msikie Dora
Akizungumza hivi karibuni akiwa nyumbani kwake Bagamoyo, Dora alisema:
“Nilihamia Bagamoyo nikitokea Mwanza, nikakutana na mwanaume anayeitwa Pascal, tukakubaliana tuishi kama mke na mume.
“Baada
ya kukubaliana hilo, nikapata ujauzito lakini nikashangaa siku moja
akaja mwanamke na kusema yeye ni mzazi mwenzake na Pascal.
“Alifanya
vurugu, akanijeruhi kisha akachukua TV na vitu vingine, akaondoka huku
akiniambia lazima nijifungue kiumbe cha ajabu. Nilipata hofu kubwa, mara
nikaanza kusumbuliwa na tumbo, nikapelekwa kwa mganga ambapo niliambiwa
nimerogwa.
“Nikatibiwa kisha nikafungwa kitambaa chenye dawa mkononi na kuambiwa nisikivue.
“Siku
moja kikapotea kimaajabu, baadaye tukakiona juu ya mti nje ya nyumba.
Nikaachana na masuala ya kienyeji, nikaamua kwenda kanisani, hata hivyo
mauzauza hayakuisha,” alisema Dora na kuongeza:
“Siku
uchungu uliponijia nikiwa Dodoma, ndugu zangu na wakunga wakaja
kunisaidia lakini cha ajabu wakashangaa kuona nazi ndiyo inatoka.
“Wakakimbia
na kuniacha nikipandisha mashetani, akaitwa mganga wa kienyeji lakini
naye aliogopa ndipo nikapelekwa kwa walokole kuombewa.
“Nilipopata
nafuu na kurudishwa nyumbani, polisi wakaja na kutuambia eti tumetupa
mtoto, wakasachi hawakuona kitu, wakatupeleka kituoni.
“Huko
nako nikapandisha mashetani, nilipotulia nikapelekwa hospitali ambako
nilisafishwa lakini ishu ikawa kubwa, polisi wakatuchukua mimi na mume
wangu na kutuweka ndani, tulitoka baada ya kutoa pesa.
“Cha
ajabu niliporudi nyumbani ili nichukue kadi niende kliniki, nikakuta
shanga kibao, ndipo tukaona cha msingi ni kurudi Bagamoyo na kuhama pale
tulipokuwa tunaishi,” alisema Dora huku akiungwa mkono na mumewe,
Pascal.
Imeandaliwa na Chande Abdallah na Deogratius Mongela