Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(CHADEMA) Ndugu FREEMAN MBOWE amefikishwa kituo cha polisi leo asubuhi
tarehe 11/04/2015 kwa kosa la kumtumia ujumbe mfupi wa maneno SMS alie
kua mbunge wa KIGOMA kaskazini kupitia Tiketi ya Chadema ndugu ZITTO
ZUBERI KABWE ambae kwasasa ni mwanachama wa ACT WAZALENDO.
Kwa mujibu wa ZITTO KABWE hakufurahishwa na kauli za maandishi yaliyo andikwa katika ujumbe huo na kikubwa zaidi kilichopelekea ZITTO KABWE kutoa taarifa polisi ni kauli iliyoandikwa katika SMS hiyo ikimuelezea ZITTO KABWE kua ni Kibaraka wa CCM na chama cha ACT wamekianzisha kama daraja la kuvuka kwa yeye kwenda CCM.
Kwa mujibu wa maelezo ya Zitto Kabwe alipo wasiliana na waandishi wa habari kutoka kituo cha BBC alisema kua
"NIMEPOKEA UJUMBE WA SMS KATIKA SIMU YANGU UJUMBE AMBAO SIO
MZURI KIUKWELI NA UJUMBE UNAONESHA KUA UMETOKA KWA MWENYEKITI WA CHADEMA
FREEMAN MBOWE NAAMINI UJUMBE UMETOKA KWAKE KWAKUA NAMBA YAKE YA SIMU
NINAYO NA NILI SAVE KATIKA SIMU YANGU YA MAWASILIANO KWA JINA LA MKT.
MBOWE KWA MAANA YA MWENYEKITI MBOWE HIVYO NILIVYOPATA UJUMBE JINA
LILITOKEA HILO LA MTUMAJI NA KUJUA UJUMBE UMETOKA KWAKE NA NILIPO
ANGALIA CENTER NUMBER IMETUMIKA YA VODACOM NIKAJARIBU KUMPIGIA HAKUA
AKIPOKEA SIMU ZANGU LENGO LA KUMPIGIA NI KUTAKA KUPATA USHAHIDI NA
UHAKIKA ZAIDI WA SAUTI YAKE LAKINI HAKUA AKIPOKEA SIMU ZANGU NDIPO LEO
ASUBUHI NIKAWASILISHA HII KESI KATIKA VYOMBO VYA SHERIA ILI KUWEKA
USALAMA JUU YA JAMBO HILI NIMEUMIA SANA KUAMBIWA MIMI NI KIBARAKA WA CCM
PIA NIMEAMBIWA KUA NIMEJIUNGA ACT WAZALENDO KAMA DARAJA TU KUWAHADAA
WANANCHI ILI NIHAMIE CCM"Hayo ndio maneno ya ZITTO KABWE. Alipo tafutwa Freeman Mbowe alizungumza haya yafuatayo
"KWA SASA SIPO TAYARI KUZUNGUMZIA HILO KATIKA VYOMBO VYA HABARI
YEYE ZITTO SI AMELIPELEKA KATIKA VYOMBO VYA USALAMA? BASI NAOMBA
TUWAACHIE WANASHERIA WAFANYE KAZI YAO." Haya ndio yaliyojiri leo asubuhi kwa wanasiasa wa Tanzania.
chanzo-hapa
Social Plugin