Hili
tukio huenda likakushtua kutokana na mazingira ambapo limetokea, sawa
tunaenda Hospitali kutibiwa lakini wale wanaotoa huduma wakati mwingine
wanakuwa na mambo yao tofauti.
Hii story unaambiwa imetokea Uingereza, Andrew Hutchinson ni nesi wa kitengo cha dharura Hospitali ya John Radcliffe Uingereza, amekutwa na hatia ya kuwabaka wagonjwa watatu walioenda kupatiwa matibabu katika Hospitali hiyo.
Muuguzi huyo anadaiwa kuwabaka wagonjwa
hao waliofikishwa kwenye Hospitali hiyo wakiwa wamepoteza fahamu,
halafu akakutwa na picha na video alizojirekodi wakati akifanya kitendo
hicho.
Polisi walipomkamata walikagua simu
yake, computer na camera na kukuta picha hizo..
Mtuhumiwa anashikiliwa
na bado uchunguzi unaendelea kwani jamaa imeonekana ana kesi pia ya
kubaka watoto wawili.
Wanawake waliofanyiwa vitendo hivyo hawakujua chochote kwa kuwa jamaa aliwaingilia wakiwa hawana fahamu.
Social Plugin