Labda
ulishtushwa na ile ya bibi harusi kujioa, kisa umri unaenda na
hajaolewa ..! Kuna ile nyingine ya mapacha kuolewa siku moja na mabwana
watatu ambao hata wao walikuwa wakiwachanganya siku ya harusi, labda
hiyo ilikufurahisha.. nyingine ilikuwa ya mwanamke kufunga ndoa na paka
wake.
Ya leo itakushangaza pia.. eti ndoa ya binadamu na nyoka?
Iko kwenye HEADLINES toka India, inamhusu Sandeep Patel ambaye alipanga mikakati ya kumuoa nyoka aina ya cobra .. anasema huyo ndio mwanamke mrembo ambaye alikuwa na ahadi nae kwamba atamuoa siku ya Pasaka.
Watu walitaka hii isiwapite yaani,
unaambiwa zaidi ya watu 12,000 walisogea kwenye hekalu ambako ndoa
ilikuwa inafanyika katika kijiji cha Badwapur, India.
Muda ulipofika taratibu zote zikaanza
kama kawaida.. mhubiri wa kihindi aliyekuwa anafungisha ndoa hiyo
aliwaambia watu kuwa jamaa huyo alikuwa anapenda nyoka tangu akiwa
mtoto.. alikuwa anatembea, anakula na kuchezesha ulimi wake kama
anavyofanya nyoka.
Polisi waliingia kwenye ukumbi huo na
kuzuia harusi hiyo isiendelee, wakawakamata bwana harusi pamoja na baba
yake.. alafu wakaanza kazi nyingine ya kuwatawanya watu wote
waliokusanyika kushuhudia tukio hilo la kihistoria.
Hii inafanana na ile nyingine ambayo imetokea Mexico, jamaa alikaa kwenye HEADLINES kwa kuoa mamba.
Social Plugin