Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

Makubwa ya PASAKA!! ALIZIDIWA NA MAHABA YA NYOKA,HARUSI IKAPANGWA,KILICHOTOKEA NI STORI!!

midigama-feb-11_183-post 

Labda ulishtushwa na ile ya bibi harusi kujioa, kisa umri unaenda na hajaolewa ..! Kuna ile nyingine ya mapacha kuolewa siku moja na mabwana watatu ambao hata wao walikuwa wakiwachanganya siku ya harusi, labda hiyo ilikufurahisha.. nyingine ilikuwa ya mwanamke kufunga ndoa na paka wake.

Ya leo itakushangaza pia.. eti ndoa ya binadamu na nyoka?

Iko kwenye HEADLINES toka India, inamhusu Sandeep Patel ambaye alipanga mikakati ya kumuoa nyoka aina ya cobra .. anasema huyo ndio mwanamke mrembo ambaye alikuwa na ahadi nae kwamba atamuoa siku ya Pasaka.

Watu walitaka hii isiwapite yaani, unaambiwa zaidi ya watu 12,000 walisogea kwenye hekalu ambako ndoa ilikuwa inafanyika katika kijiji cha Badwapur, India.

Muda ulipofika  taratibu zote zikaanza kama kawaida.. mhubiri wa kihindi aliyekuwa anafungisha ndoa hiyo aliwaambia watu kuwa jamaa huyo alikuwa anapenda nyoka tangu akiwa mtoto.. alikuwa anatembea, anakula na kuchezesha ulimi wake kama anavyofanya nyoka.
.
Sandeep Patel akiwa na nyoka wake.

Polisi waliingia kwenye ukumbi huo na kuzuia harusi hiyo isiendelee, wakawakamata bwana harusi pamoja na baba yake.. alafu wakaanza kazi nyingine ya kuwatawanya watu wote waliokusanyika kushuhudia tukio hilo la kihistoria.

Hii inafanana na ile nyingine ambayo imetokea Mexico, jamaa alikaa kwenye HEADLINES kwa kuoa mamba.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com